Monday, November 25, 2013

Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema  ziara ya ujumbe wa watu zaidi ya 70 kutoka  Serikali za Mitaa nchini  China  utasaidia kukuza uchumi wa  Tanzania  na  kuendeleza ushirikiano baina ya  nchi hizo  hadi kwa  manufaa ya wananchi.
Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri Mkuu Mizengo Pinda  wakati akifungua  majadiliano hayo kwenye  ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa  Mwalimu  Julius .K. Nyerere jijini Dares Salaam.
“Ziara hii itasaidia kujenga uwezo kwa kusimamia shughuli za Serikali za Mitaa kwa pamoja    kuboresha ushirikiano ,kukuza uchumi   na ushirikiano wa kibiashara na maendeleo ya  sekta binafsi kupitia fursa za biashara, uwekezaji na viwanda kwa manufaa ya  wananchi wa nchi hizi mbili.
 Alisema Tanzania kio tayari kufanya kazi kwa pamoja  na  ujumbe huo, hivyo aliwataka viongozi mbalimbali wa Serikali za  Mitaa nchini  kutumia fursa kwa kubuni maeneo ya uwekezaji.
 Kwa upande wake Kiongozi wa msafara huo, Naibu Gavana wa Jimbo la  Shandong , Xia  Geng, aliyataja  maeneo ya ushirikiano kupitia ziara hiyo ni , shughuliza kiuchumi, biashara,  nishati na huhifadhi wa mazingira.
 Naye Balozi wa China nchini, Lu Youqing alisema serikali ina nafasi ya kutengeza ajira kwa wananchi,  hivyo aliishauri viongozi wa Serikali za Mitaa  nchini kuliangalia suala hilo.
 Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali(TAMISEMI), Hawa Ghasia  alisema  alitembelea China mwaka jana akiwa na timu yake ambapo  wamejifunza kuwa , wana maendeleo mazuri katika masuala ya serikali za mitaa.
 Aliongeza kuwa maendeleo hayo yamewafanya kutotegemea vyanzo vya fedha kutoka Serikali Kuu wala rasilimali watu, inapanga,inaogeza na  kutumia vyanzo vyake vya mapato kwa usimamizi mdogo wa Serikali na kukopa fedha kutoka taasisi mbalimbali za kifedha.
 Waziri huyo alisema pia inahusishisha jamii katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo
Ujumbe wa watu wapatao 70  kutoka   Serikali za Mitaa kutoka China, wakiwemo magavana,mameya na wafanyabiashara ambao  umekuwepo kwa ziara ya siku  nne kwa  ajili ya majadiliano hayo na  mawaziri wa Sekta mbalimbali, wakuu wa Mikoa,  wakuu wa Wilaya, makatibu Tawala wa Mikoa.
Wengine ni baadhi ya Mameya/Wenyeviti wa Halmashauri za Jiji, Manispaa, Miji na Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri,Taasisi za Serikali na Binafsi  pamoja na Wafanyabiashara.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video