JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mamlaka
ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) inasheherekea maadhimisho ya miaka 10
tangu kuanzishwa kwake huku yakiwemo mafanikio makubwa dhahiri na ya
kujivunia katika sekta ya mawasiliano nchini.
TCRA
ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 23 mwezi Novemba mwaka 2013 ili
kusimamia Sekta ya Posta na Mawasiliano ya Elektroniki ikkiwemo simu,
utangazaji, wavuti pamoja na huduma za Posta. TCRA ilkianzishwa kwa
Sheria Na. 12 ya mwaka 2003 iliyoziunganisha Tume ya Mawasiliano
Tanzania (TCC) na Tume ya Utangazaji Tanzania (TBC).
Mkakati
mahususi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ni “Kuboresha Maisha ya
Watanzania kupitia mfumo makini na thabiti ili kuhakikisha kunakuwa na
huduma za mawasiliano kwa wote nchini”. Katika kipindi cha miaka kumi
iliyopita, Tanzania imeshuhudia kukua kwa kasi kwa Sekta ya Mawasiliano.
Mamlaka ilianzisha mfumo wa leseni za Muingiliano mnamo tarehe 23
Februari 20005.
Mfumo
huu wa leseni za muingiliano (Convergence Lisensing Framework) umekuwa
chachu ya kuongezeka kwa miundombinu mbalimbali ya mawasiliano, huduma
mbalimbali kwa kutumia mtandao wa mawasiliano ikiwemo wavuti (internet)
na utangazaji.
Makampuni
ya simu yameongezeka kutoka kampuni moja ya simu TCRA ilivyoanzishwa
mwaka 2003 hadi kufikia makampuni saba (7) yenye wateja wenye laini za
simu takribani milioni 28 kulinganisha na idadi iliyokuwepo miaka kumi
iliyopita. Huduma za simu za mkononi zimebadilisha maisha ya Watanzania
kutokana na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia simu za mkononi.
Kuanzia huduma za kutuma fedha kupitia simu, malipo ya Ankara mbalimbali
na huduma nyingine nyingi zilizobadilisha maisha na uchumi wa wananchi
wa taifa hili.
Sekta
ndogo ya Posta nayo haijabaki nyuma kwani kumekuwepo na ongezeko la
watoa huduma kutoka mmoja hadi zaidi ya hamsini wenye kutoa hduma ndani
nan je ya Tanzania. Tunatarajia mabadilikjo makubwa kwa watanzania hasa
baada yan kukamilika kwa mradi wa anwani mpya za makazi na misimbo ya
Posta.
Hali
kadhalika, yako mabadiliko makubwa sana katika msekta ndogo ya
utangazaji. Kutoka nchi yetu kuwa na Radio moja hadi Zaidi ya redio 85.
Aidha kutokuwepo kwa Kituo cha Utangazaji wa Runinga hadi vituo vya
utangazaji vipatavyo 26. Watumiaji wa wavuti (intanet wameongezeka
kutoka watumiaji million moja hadi takribani milioni 8 na ushee. Sekta
ya Mawasiliano imekuwa chimbuko la maendeleo ya nchi kwa kutoa ajira kwa
watanzania wengi na hali kadhalika kuongeza mapata ya serekali kwa tozo
na kodi mbalimbali zinazotolewa katika sekta..
Mamlaka
ya Mawasiliano imeshinda tuzo mbalimbali katika masuala ya Udhibiti na
Usimamizi Bora wa Huduma za mawasiliano nchini katika kipindi cha kuweko
kwake miaka kumi iliyopita. Nchi mbalimbali zimekuja Tanzania kujifunza
udhibiti na usumamizi wa masuala nyeti ya mawasiliano kama vile masuala
ya uhamaji kuelekea mfumo mpya wa utangazaji wa dijitali, Mifumo ya
uanzishwaji wa anwani za makazi na misimbo ya posta, Usimamizi mzuri wa
masafa na namba za mawasiliano na mambo mengine mengi.
MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MAADHIMISHO TANGU 25 – 29 NOVEMBER 2013
Katika
kusheherekea miaka kumi ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, kutakuwa na
maadhimisho ya wiki nzima yenye matukio mbalimbali. Tukianzia na
mkutano huu na waandishi wa habari uliokusudia kutoa taarifa kwenu na
kwa wananchi kuhusu maadhimisho haya, kutakuwa na matukio kadha wa kadha
kuelekea kilele cha sherehe za maadhimisho yanayotarajiwa kufanyika
tarehe 29 Novemba 2013.Maadhimisho haya yanafanika chini ya kauli mbiu
ya; Miaka 10 ya TCRA: Miaka Kumi ya Mapinduzi Katika Sekta ya
Mawasiliano
Kesho
tarehe 26 Novemba 2013 kutakuwa na tukio maalumu kwa wafanyakazi wa
mamlaka ambapo wale waliokuwepo tangu wakati wa kuanzishwa kwa TCRA
watatunukiwa vyeti pamoja na zawadi mbalimbali kutambua mchango wao kwa
taasisi.
Aidha
siku ya tarehe 27Novemba 2013; kutakua na sherehe ya kutoa udhamini kwa
wanafunzi wanaosoma vyuo vya elimu ya juu wanaochukua masomo ya
mawasiliano, sayansi na teknolojia. TCRA kwa kipindi cha miaka miwili
mfululizo imekuwa ikitoa udhaminim katika masomo hayo kwa wanafunzi
mahiri kwa nia ya kukuza weledi na kuboresha utumishi katika sekta ya
mawasiliano chini ya kinachoitwa “TCRA ICT SCHOLARSHIPS” kwa wanafunzi
wa digrii ya kwanza, digrii za Uzamili na Uzamivu.
Kuanzia
tarehe 27 – 29 Novemba, kutakuwa na maonesho maalumu katika viwanja vya
ukumbi wa mikutano wa Mlimani City ambapo watoa huduma mbalimbali za
mawasiliano nchini wataonesha mafanikio yao na huduma wanazotoa kwa
wananchi. Napenda kuchukua fursa hii kuwasihi waandishi wa habari
kuhudhuria maonesho haya ili kujifunza na kutumia fursa hiyo kuelimisha
jamii ya watanzania kuhusu huduma mbalimbali za mawasiliano
zinazopatikana nchini ili wachangamkie fursa.
Hali
kadhalika, katika maadhimisho haya, TCRA imeandaa washa maalumu ya siku
mbili wa wadau wa mawasiliano kujadili fursa, changamoto pamoja na
namna gani kwa pamoja tunavyoweza kufanya mawasiliano kuwa bora Zaidi
nchini mwetu. Warsha hiyo itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa
Mlimani City na itafunguliwa rasmi tarehe 28 mwezi huu na Mhe. Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na utaendelea hadi tarehe 29
Novemba 2013. The Opening Ceremony will be graced by Dk. Mohammed
Gharib Billal.
Wadau
mbalimbali wa Mawasiliano kama vile kituo cha Habari cha Tanzania
Network Information Centre (tzNIC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote –
Universal Communications Services Access Fund (UCSAF), Wamiliki wa
Vyombo Vya Habari – Media Owners Association of Tanzania (MoAT-
Broadcasting), na Umoja wa Makampuni ya Simu – Mobile Operators
Association of Tanzania (MoAT-Mobile Telephony Companies), Africa Media
Group, Agape Associates and TTCL watawasilisha mada mbalimbali.
Vyombo
vya Habari vinakaribishwa katika shughuli zote za maadhimisho ya Miaka
10 ya TCRA ili kutoa elimu kwa umma lakini pia kama fursa ya kujionea
mafanikio ya sekta ya mawasiliano katika kipindi cha miaka kumi
iliyopita ili kuwawezesha wananchi kufahamu tulikotoka, tunakoenda na
fursa zilizoko katika sekta ili kuboresha maisha yao.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
25th November 2012


0 comments:
Post a Comment