Friday, November 29, 2013

SONY DSC
Kocha wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
WAKATA miwa wa mashamba ya Manungu Turiani Mkoani Morogoro, wenyewe wanaita Mji kasoro bahari, wana TamTam Mtibwa Sugar kuanza mawindo yao ya mzunguko wa pili desemba 10 mwaka huu.
Mwenyekiti wa klabu hiyo, Jamal Bayser amesema mipango imekaa sawa na ifikapo siku hiyo wachezaji wote watatakiwa kuripoti mazoezini ili kuendelea kujiimarisha zaidi kabla ya kuanza ngwe ya lala salama.
“Mipango yetu ni kuhakikisha tunafanya vizuri, na ndio maana tutaanza tarehe za mapema ili kumpa muda wa kutosha kocha wetu, mecky Mexime kusuka kikosi chake ili kuwa na nguvu zaidi za kusaka nafasi nzuri”. Alisema Bayser.
Bayser alisema kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha wao, hawatakiwa kusajili mchezaji yeyote kwani kikosi kina nyota wa kutosha.
“Mwalimu alisema wachezaji alionao wanamtosha, hivyo nasisi hatujasajili kabisa katika dirisha hili dogo, lakini uhakika ni kuwa Mtibwa inao wachezaji wengi na wazuri. Ikumbukwe sisi tumekuwa tukizalisha wachezaji wazuri kwa wakati wote wa ushiriki wa ligi kuu”. Alisema Bayser.
Akizungumzia kuondoka  kwa Issa Juma Awadh aliyejiunga na Simba SC katika dirisha dogo la usajili, Bayser amesema hawana shida kwani mara nyingi timu kubwa zimekuwa zikiwanasa nyota wao, lakini bado wanaendelea kutengeneza wengine wazuri zaidi.
“Sisi Mtibwa sio watu wa kukurupuka, tuna utulivu mkubwa inapofika wakati wa usajili, matunda yanaonekana na ndio maana hawa wanaojiita wakongwe wa soka la Tanzania wanakodolea macho kwetu”.Alisema.
Mtibwa Sugar waliwahi kuwa mabingwa mara mbili mfululizo wa ligi kuu, mwaka 1999 na 2000, lakini miaka ya karibuni wamekuwa washiriki zaidi kwani wanashindwa hata kuingia nafasi tatu za juu licha ya historia yao nzuri katika michuano hii ya ligi kuu soka Tanzania bara.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video