![]() |
| Alex Msama |
Na Mwandishi Wetu
WAANDAAJI
wa Tamasha la Krismas wametangaza kuwa tamasha hilo litafanyika Uwanja
wa Taifa, Dar es Salaam Desemba 25 mwaka huu, pia litafanyika Mikoa ya
Tanga na Arusha.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa Kamati ya
Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ilieleza kuwa baada ya kumalizika
maonesho ya Dar es Salaam, Desemba 26 itakuwa Uwanja wa Jamhuri,
Morogoro na Desemba 28 Uwanja wa Mkwakwani Tanga na siku inayofuata
Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Alisema
awali pia walipokea maombi kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki wa
Injili nchini wakiomba lifanyike katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na
Mbeya, Mwanza, Shinyanga na Zanzibar.
“Kwa
sasa tumepitisha mikoa hiyo minne, tunaomba wadau wetu watuunge mkono,
tunaamini litakuwa tamasha la aina yake kutokana na aina ya wasanii
tulio nao,” alisema Msama.
Tamasha
la Krismas linaandaliwa na Kampuni ya Msama Promotion ya jijini Dar es
Salaam, ambayo pia huandaa Tamasha la Pasaka kila mwaka.
Kwa
mujibu wa Msama wanataka Tamasha la Krismas liwe bora zaidi kuliko la
Pasaka kwa kualika wasanii maarufu kutoka nje na ndani ya Tanzania.
Alisema
hilo litakuwa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu na litakuwa na
tofauti kubwa iilinganisha na matamasha mengine yaliyowahi kuandaliwa na
kampuni yake.


0 comments:
Post a Comment