SHABANI KAONEKA |
MABONDIA Said Mbelwa na Shabani Kaoneka wamesainimakubaliano ya kupambana siku yaNovember10 katika ukumbiwa Zulu Paradise uliopo pugu Kirumba Dar es salaam.
Akizungumzia mpambano huo kocha wa kimataifa wa masumbwi ambaye ni mratibu
wa mpambano huo , Rajabu Mhamila ‘Super D’ ‘amesema kuwa mpambano huo
uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki kutokana na majigambo ya
mabondia kutafutana kwa muda mrefu.
Mpambano
huo wa raundi 8 umekuwa gumzo katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar
es salaam kama vile Chanika, Ilala, Manzese, Mabibo na Kinondoni
kutokana na umahiri wa mabondia wenyewe.
katika mchezo huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi ambapo bondia
Twaribu
Mchanjo ataoneshana kazi na Mohamedi Kashinde uku Chilambo Hemed
akivaana na Sharif Mzezele na bondia machachari Hamza Mchanjo
akioneshana umwamba na Tonny Kabeo, bondia tishio katika uzito mwepesi
Adamu Ngange atapambana na Shabani Mtengela na Said Uwezo akichuana
na Paul Rabiano
Mpambano huo wenye ushinani wa kila pande za jiji unatarajia kutikisa jiji kutokana na mabondia wote kuwa na viwango vya juu.
Pia siku hiyo kutakuwa na uzinduzi rasmi wa DVD za bondia Said Mbelwa akicheza nje ya nchi na bondia Hamid Rahimi lililofanyika Loya Gerga, Kabul, Afghanistan jingine ni kati yake na Balazs Kelemen lililofanyika katika ukumbi wa
Messzi
István Sporthall, Kecskemet, Hungary pamoja na lile lililofanyika
katika ukumbi wa Sporthall, Galanta, Slovakia akipambana na Tamas Kovacs na mpambano mwingine aliyecheza na Bernard Donfack katika ukumbi wa
Saarlandhalle, Saarbruecken, Saarland, Germany
mapambano yote hayo makubwa
ni
kwa ajili ya kuwaonesha mabonia wa Tanzania kuwa ukikazania mchezo wa
masumbwi pia unaweza kukutoka kimaisha na kukufanya uzunguke dunia kwa
ajili ya kushiliki michezo mbalimbali ya masumbwi Duniani
Mbelwa
kwa sasa ndie bondia anaetamba katika kusafili kwa kushiliki mashindano
mengi ya nchi za nje kutokana na kukubalika kwake na kujijengea
mahusiano mazuri na nchi mbalimbali alizowai kwenda kushiliki mashindano
makubwa likiwemo lile la Kabul, Afghanistan
lililofanyika kwa ajili ya kurudisha amani nchini humo
DVD
hizo na nyingine mbali mbali zitakuwa zikiuzwa kama mpambano wa EVANDER
HOLYFIEL VS RIDDICK BOWE YA TAREHE 13,NOVEMBA,1992,MUHAMMAD ALI VS
JOE FRAZIER
Manny Paquaio, Saul ‘canelo’ alverez ,Floyd Mayweathar,Mike Tyson,Mohamed Ali,Ferex Trinidad,Miguel Cotto na wengine wengi
DVD hizo za ngumi kali zitakuwa zikiuzwa na kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila ‘Super D’
Pamoja
na kutambua sheria na taratibu za mchezo huo siku hiyo pia kuta kuwa na
vifaa vya mchezo huo wa masumbwi vitakavyotolewa zawadi kwa mabondia
na Kocha Super D ambaye ameweka ahadi ya kugawa, Gum Shit ,Clip
Bandeji,DVD za Mafunzo kwa mabondia, Bukta,Protector na vifaa mbalimbali
kwa mabondia watakao onesha uwezo wa ali ya juu wa kutupiana masumbwi
DVD
KWA SASA ZINAPATIKANA MAKUTANO YA BARABARA YA UHURU NA MSIMBAZI DAR ES
SALAAM KARIAKOO ZAIDI WASILIANA NA SUPER D SUPER COACH KWA NAMBA YA SIMU
0713406938 Rajabu Mhamila ‘Super D’
0 comments:
Post a Comment