Saturday, November 2, 2013


Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
Raundi ya 12 ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) imeendelea leo (Novemba 2 mwaka huu) kwa mechi nne kuchezwa  katika  katika miji minne tofauti.
Azam fc wana `Lambalamba` wamerejea tena kileleni leo hii na kuwashusha Yanga waliokuwa wakiongoza kwa pointi 25 baada ya kupata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Ruvu Shooting, uwanja wa Azam Complex, Chamaz, Dar es salaam na kukalia usukukani  kwa kujikusanyia pointi 26 sawa na Mbeya City ambao nao leo hii wameshinda bao 1-0 dhidi ya Ashanti United Uwanja wa sokoine , Mbeya, lakini wanazidiana mabao ya kufunga na kufungwa.
Hadi mapumziko, Azam FC walikuwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyotiwa nyavuni kupitia kwa  Kipre Herman Tchetche katika dakika ya kwanza tu ya mchezo baada ya kuwachomoka mabeki wa Ruvu Shooting  na kinda Joseph Kimwaga aliyepandishwa kutoka timu ya vijana msimu huu, alifunga bao lake katika dakika ya 45 akiunganisha kichwa krosi iliyochongwa na beki , Waziri Salum.
Picha ya 24 
Kipindi cha pili, Azam walianza soka kwa umakini mkubwa na uangalifu  mkubwa na dakika ya 70 Khamis Mcha `Vialli` alifunga bao la tatu kwa shuti kali baada ya kumtoka beki wa Ruvu Shooting.
Kikosi cha Azam FC leo: Mwadini Ally, Erasto Nyoni, Waziri Salum, Said Mourad, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha, Himid Mao/Jabir Aziz dk58, Kipre Tchetche, Humphrey Mieno na Joseph Kimwaga/Farid Mussa dk69.
Ruvu Shooting: Abdul Seif, Michael Pius, Stefano Mwasyika, Mangasini Mbonosi, Shaaban Suzan, Juma Dion, Juma Nade, Hassan Dilunga, Saidi Dilunga, Elias Maguri na Cossmas Lewis
DSC003801 
Huko Mbeya wenyeji wa uwanja wa Sokoine, Mbeya City wamejikusanyia pointi tatu na kurejea nafasi ya pili katika msimamo baada ya ushinidi wa bao 1-0 dhidi ya wauza Mitumba wa Ilala, Ashanti United.
Bao hilo limetokana na krosi iliyochongwa na beki wa kushoto wa Mbeya City, Hassan Mwasapili katika dakika ya 30 na katika harakati za kuokoa mchezaji wa Ashanti  Samir said Ruhava  alijifunga.
Hata hivyo shuhuda wa mtandao huu pale jijini Mbeya, Laudens Simkonda Galimoshi ameeleza kuwa, Mbeya City leo walibanwa sana na wameshindwa kuonesha kasi yao mbele ya watoto wa mjiji.
Alisema kuwa baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Mbeya City,  Juma Mwambusi amekiri timu yake kutocheza vizuri ingawa ameweka bayana kuwa  mechi za mfululizo zimeathiri kikosi chake.
Huko Uwanja wa Manungu Complex mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wameshinda bao 1-0 dhidi ya JKT  Oljoro.
Bao pekee la Mtibwa  Sugar limefungwa na  Salim Mbonde na kuwapa raha mashabiki wa Mtibwa waliofurika katika uwanja huo.
Huko dimba la CCM Mkwakwani jijini Tanga, Mgambo walioneshana kazi na Coastal Union na mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zimetoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Raundi hiyo itakamilika kesho Novemba 3 mwaka huu kwa mechi moja ambapo Tanzania Prisons itakuwa mwenyeji wa Oljoro kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Mechi za kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo zitachezwa Novemba 6 na 7 mwaka huu. Novemba 6 ni JKT Ruvu vs Coastal Union, Ashanti United vs Simba, Kagera Sugar vs Mgambo Shooting, na Ruvu Shooting vs Mtibwa Sugar.
Novemba 7 mwaka huu, Azam itacheza na Mbeya City, Yanga itacheza na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Rhino itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video