Friday, November 29, 2013

RUVU SHOOTING 
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe, Dar es salaam
MAAFANDE wa jeshi la kujenga Taifa kutoka wa mkoani Pwani, Ruvu Shooting Stars wameendelea wamesisitiza nia yao ya kuongeza nyota kadhaa ili kuimarisha kikosi chao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi kuu soka Tanzania bara mwezi januari mwakani.
Kocha Mkuu wa klabu hiyo, Charles Boniface Mkwasa `Masta` amezungumza na mtandao huu na kueleza kuwa mpaka sasa hawezi kusema anamsajili nani, lakini mchakato unaendelea na muda wowote atatoa taarifa kwa vyombo vya habari.
“Nilishawasilisha mapendekezo yangu, viongozi wapo hatua za mwisho kulishughulikia suala hili. Lazima niongeze nguvu sehemu ya Mlinda Mlango na ushambuliaji kwani mzunguko wa kwanza tuliruhusu mabao mengi na kukoasa nafasi nyingi za wazi, hii inaashiria kuwa maeneo hayo kuna udhaifu”. Alisema Mkwasa.
Mkwasa aliongeza kuwa wanatakiwa kufanyia kazi pia sehemu ya kiungo hasa baada ta kuondoka kwa nyota wao kinda Hassan Dilunga aliyetimkia kwa mabingwa watetezi na vinara wa ligi hiyo, Dar Young Africans.
Kocha huyo alisema mzunguko wa pili utakuwa mgumu sana kwani kila timu inajiwinda, lakini atafanya kila linalowezekana kuwa na kikosi bora cha kuhimili vishindo vya wapinzani.
“Nipo katika wakati wa mpito kusuka kikosi changu, tuna madhaifu kadhaa, lakini nitayarekebisha ili kuendana na kasi ya ligi kuu mzunguko wa pili”. Aliongeza Mkwasa.
Msimu uliopita Ruvu shooting ilimwagiwa sifa nyingi wa  wapenda soka nchini kwa kuonesha kiwango kizuri sana, lakini msimu wa mwaka huu wanaonekana kuwa na makosa mengi hasa sehemu ya ulinzi na ushambuliaji.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video