Mkuu
wa Mkoa akiwa amekaa juu ya dawati lililotengenezwa na wananchi wa
Kata ya Nenkwa Tarafa ya Inyonga kwa kutumia nguvu zao ikiwa ni kuunga
mkono serikali kuondoa tatizo hilo ili watoto wasiendelee kuka chini.
Mzee
wa Kabila la kipimbwe mkazi wa kijiji cha Mamba ambaye jina
halikufahamika mara mmoja akimzawadia Mkuu wa Mkoa Mbuzi Mnyama ikiwa
ni Ishara ya upendo kwake kwa kuonesha furaha kufika kuwatembelea kijiji
kwao na kuhimiza shughuli za maendeleo
Mkuu
wa MKOA WA KATAVI DKT Rajabu Rutengwe akikagua ujenzi wa mnada katika
kijiji cha majimoto na kukuta umejengwa chini ya kiwango na kuagiza
mradi huo urudiwe tena
(Picha Na Kibada Kibada Katavi)
Na Kibada Kibada -Katavi
Serikali
Mkoani Katavi imepiga marufuku watu kuishi kwenye maeneo yasiyoruhusiwa
na kuwataka waondoke mara moja ama sivyo watachukuliwa hatua kali za
kisheria iwapo watakaidi.
Hatua
hiyo imekuja siku chache kupita baada ya kuondolewa wale wote waliokuwa
wakiishi maeneo ya hifadhi ya wanyama pori ya taifa ya Katavi na kwenye
maeneo ya vyanzo maji huku wakifuga na wengine kuendesha shughuli za
kijamii kama kulima na shughuli nyingine.
Watu hao wote wametakiwa kuondoka kwa kuwa walikuwa wamekwishaondolewa
kufuatia operation tokomeza ujangili iliyofanyika mwezi oktoba mwaka na
kuwaondoa wengine wameanza kurudi katika maeneo hayo.
Kufuatia
kuwepo kwa tetesi kuwa wapo baadhi ya wananchi hususani wafugaji kuanza
kurejea katika maeneo hayo wakiwa na makundi yao ya mifugo, Mkuu wa
Mkoa ametoa agizo la kuondoka haraka katika maeneo hayo na kusisitiza
kuwa wasidanganywe na wanasheria uchwala kuwa watawatete pindi watakauwa
wamevunja sheria hizo.
Aidha
Mkuu huyo wa Mkoa alipata nafasi ya kutembelea baadhi ya maeneo
yaliyoondolewa wananchi na wengine wameanza kurejea na kukutana na
makundi ya mifugo na kuagiza waondoke.
Akiwa
katika moja ya mikutano yake ya hadhara katika maeneo mbalimbali
alipokea malalamiko kutoka kwa wananchi wa Tarafa ya Mamba Wilayani
Mlele wa Vijiji vya Kata za Ikuba, Mede, Majimoto Usevya na Mamba kuwa
waliondolewa na kuchomewa nyumba zao wakati wa operation tokemeza
ujangili ilipokuwa ikiendelea jambo ambalo walidai walionewa wakaomba
kurudi kwenye maeneo hayo waliyoyaita yao.
Wananchi
hao walieleza kuwa wao walikwenda kuishi huko kwa maelekezo waliyopewa
na badhi ya viongozi wa serikali za vijiji kwa kuuziwa maeneo hayo
ambayo baadhi yao yako ndani ya hifadhi ya wanyama na mengine yako
kwenye vyanzo vya maji ambavyo vimeharibiwa kutoka na shughuli za
kibinadamu kama kilimo ufugaji, ukataji miti, na nyinginezo ziliathiri
kwa kiasi kikubwa maeneo hayo.
Akitoa
taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi Dkt Rajabu Rutengwe ya operation
tokomeza majangili iliyofanyika wilayani Mlele, Mkuu wa Wilaya hiyo
Kanali Ngemela Lubinga alieleza kuwa katika operation hiyo iliyoanza
oktoba 14 mwaka huu kwa kujumuisha askari wa Jeshi la wananchi Tanzania(
JWT) askari polisi,Usalama wa Taifa wataalamu toka Halamshauri na
askari wa Hifadhi ya Rukwa /Lukwati jumla ya kaya 577 ziliondolewa ndani
ya maeneo ya hifadhi ya Taifa ya Katavi,
Katika
operation hiyo silaha tisa zikiwemo (SMG ) nne zilisalimishwa na
nyingine 150 zilikamatwa zoezi hilo limesaidia sana majangili na
waharibifu wa mazingira kudhibitiwa na maliasili ya nchi kulindwa
kutokana na kuwepo kwa watu waliokuwa wakiharibu mazingira na maliasili
za Taifa na wengine kuingiza mifugo katika Hifadhi za Taifa na maeneo
tengefu.
Katika
zoezi hilo la tokomeza ujangili kwa wilaya ya mlele maeneo yaliyoguswa
ni Kata za
Ilunde,Mapili,Ikuba,Ugalla,Sitalike,Mwamapuli,Mamba,Machimboni,na
Itenka,kwa wananchi waliokuwa wakiishi ndani ya maeneo yasiyoruhisiwa na
wengine ndani ya hifadhi na vyanzo vya maji.
Hivyo
Mkuu wa Mkuoa amepiga marufuku kwa mtu yeyeote kuishi katika maeneo
yaliyokatazwa na serikali badala yake waende katika maeneo yao ya vijiji
waliyopimiwa na yanayotambulika kisheria, na kusisitiza kuwa
wasidanganywe na wanasheria uchwala kuwa wakirudi katika maeneo hayo
watawasaidia .
Naye
Mkuu wa Wilaya Kanali Ngemela Lubinga amesisitiza kwa wananchi kuishi
na kufuata sheria za nchi na kufuata maelekezo yanayotolewa na viongozi
wao kuliko kuwa wajeuri kwani ujeuri hausaidii kitu, badala yake
Utaumia, Nchi inatawaliwa kwa kufuata sheria kanuni na Taratibu
zilizowekwa


0 comments:
Post a Comment