Ndege
bandia ikitayarishwa kwa zoezi la kuzima moto wa ndege uliofanyika
tarehe 21, Nov, 2013 kwenye eneo maalumu lililotengwa kwaajili ya zoezi
hili jijini Dar es Salaam. 
Baadhi
ya waokoaji wa jeshi la zimamoto wakiwa katika zoezi la uzimaji wa
moto wa ndege Nov. 21,2013 katika eneo maalumu kwa ajili ya zoezi hilo
jijini Dar es Salaam.Mazoezi hayo yamewashirikisha wanafunzi 22.
Baadhi
ya Askari wahitimu wa Jeshi la zimamoto nchini wakifanya zoezi la
kumkimbiza majeruhi kumpeleka hospitali baada ya kumuokoa kwenye
ajali.zoezi hilo limeshuhudiwa na mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani
ya Nchi, Mh.Dkt.Emannuel Nchimbi.(hayupo katika picha) Nov.21,2013
jijini Dar es Salaam.
Kikosi
cha Askari wa Jeshi la zima moto waliomaliza mafunzo ya kuzima moto wa
ndege wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo katika picha) Mh, Dkt,
Emmanuel Nchimbi, Nov, 21,2013, Wahitimu hao katika risala yao
wamesema kwamba wamepata uelewa mkubwa utakaowawezesh a kufanya
majukumu yao
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto)
akimpongeza Protacy Lichenjele(kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha
uaminifu,kwani kitendo cha askari huyo kurudisha fedha baada ya
kugundua amezidishiwa ni kitendo chenye kuhitaji moyo na uzalendo wa
kuigwa! (21 Nov, 2013)
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi (kushoto)
akimpongeza Protacy Lichenjele(kulia) baada ya kumkabidhi cheti cha
uaminifu,kwani kitendo cha askari huyo kurudisha fedha baada ya
kugundua amezidishiwa ni kitendo chenye kuhitaji moyo na uzalendo wa
kuigwa! (21 Nov, 2013)
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Dkt. Emmanuel Nchimbi(kulia) akipongezana
na Kamishna Generali wa Jeshi la Zimamoto nchini Piusi Nyambacha
(kushoto) baada ya kumalizika hafla ya kozi ya zoezi la kuzima moto wa
ndege kwa askari wa jeshi la zima moto. Nov.21,2013 jijini Dar es
Salaam.
Picha zote na MWANAKOMBO JUMAA


0 comments:
Post a Comment