Thursday, November 28, 2013


KILI STARS YAIKOMALIA ZAMBIA MICHUANO YA CECAFA, YATOKA SARE YA 1-1, BURUNDI YAWAADHIBU MABAHARIA WA SOMALIA!!

Wachezaji-wa-timu-ya-Kilimanjaro-Stars-wakishangilia-bao-dhidi-ya-Sudan 
Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
TIMU ya Taifa ya Tanzania bara, The Kilimanjaro Stars imeanza kwa sare michuano ya Mataifa ya Afrika mashariki na kati, CECAFA Challenge baada ya jioni ya leo kufungana bao 1-1 na waliowahi kuwa mabingwa wa Afrika, timu ya Taifa ya Zambia maarufu kwa jina la Chipolopopo kwenye uwanja wa Kenyatta, Machakos, Kenya.
Zambia walikuwa wa kwanza kuandika bao katiKa mchezo huo wa kundi B kupitia kwa nyota wake Ronald Kampamba dakika ya 41, akiunganishwa kwa kichwa `ndosi` krosi iliyochongwa na aliyewahi kuwa mchezaji bora wa Afrika wa Tuzo ya BBC,  Felix Katongo.
Chipolopolo walitawala zaidi mchezo huo kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi nyingi za kupata magoli, lakini umahiri wa kipa mkongwe Ivon Philip Mapunda uliiokoa stars kwani aliokoa michomo kadhaa ya Wazee wa Risasi za Shaba.
Kipindi cha pili, Kili Stars ilicheza mpira mzuri na katika dakika ya 48 walipata bao kupitia kwa beki Said Morad akiunganisha mpira wa kona uliochongwa na kiungo mahiri Salum Abubakar ‘Sure Boy’ .
Bao hilo liliwapa nguvu Stars na kuanza kusaka soka la uhakika na kuwaacha Zambia wakihaha huku na kule, lakini mlinda mlango wao, Nsabata Toaster aliwasaidia sana kwa kuokoa hatari nyingi langoni mwake.
Kikosi cha Stars kilikuwa; Ivo Mapunda, Himid Mao, Erasto Nyoni, Said Morad, Kevin Yondan, Frank Domayo, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Ramadhani Singano ‘Messi’ dk89, Hassan Dilunga/Athumani Iddi ‘Chuji’ dk85, Elias Maguri/Haroun Chanongo dk72, Amri Kiemba na Mrisho Ngassa.
Chipolopolo; Nsabata Toaster, Bronson Chama, Jimmy Chisenga/Kabaso Chongo dk67, Christopher Munthali, Rodrcik Kabwe, Stanley Nshimbi/Alex Nshimbi dk57, Sydney Kalume, Kondwani Mtonga, Felix Katongo/Salulani Phiri dk73, Ronald Kampamba na Festus Ndewe.  
Mchezo wa mapema uliwakutanisha timu ya Taifa ya Burundi dhidi ya Somalia na kushuhudia Warundi wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye uwanja wa Kenyatta, Machakos nchini Kenya.
Mabao ya Burundi yalitiwa kambani na nyota wake Abdoul Fiston dakika ya 40 na Nduwarugira Christopher dakika ya 55.
 Kwa matokeo ya mechi za leo za kundi B, Burundi wanaongoza kundi hilo kwa pointi tatu wakifuatiwa na Kili Stars na Zambia wenye pointi moja, huku wasomali wakiburuza mkia.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video