Baadhi ya washiriki wa kozi ya Ukocha Ngazi ya Pili (Intermediate)
wakimsikiliza mkufunzi wa kozi hiyo, Rogasian Kaijage (hayupo pichani)
Juni mwaka huu.Kozi hiyo iliendeshwa na DRFA.
……………………………………………………………………………………………..
CHAMA
cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) kimezitaka timu
zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha
makocha wao wanakuwa na taaluma ya ngazi ya pili (Intermediate) na
mikataba ya kazi hiyo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano wa DRFA Kenny Mwaisabula amesema Dar es Salaam
kuwa timu zote zinatakiwa kutekeleza agizo ili kuendana na malengo ya
chama hicho katika kukuza na kuendeleza mchezo huo.
“Tunazitaka
timu zote zinazoshiriki Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam kuwa
na makocha wenye taaluma hiyo Ngazi ya Pili (Intermediate), tunafanya
hivi ili kuendana na dhamira yetu ya kukuza na kuendeleza mpira wa
miguu.
“Kama
mtakumbuka vizuri DRFA iliendesha mafunzo ya ukocha wa Ngazi ya Pili
(Intermediate) Juni mwaka huu ikiwa na nia njema ya kuhakikisha
mafanikio yanapatikana, tumekuwa mstari wa mbele na mfano wa kuigwa
katika kuendeleza mpira wa miguu hasa taaluma ya makocha,” alisema.
Alisema timu hizo zimepewa mechi tatu kutekeleza agizo hilo na iwapo hawatatekeleza zitachukuliwa hatua.
Ligi Daraja la Pili Mkoa wa Dar es Salaam ilianza Novemba 23 ikishirikisha timu 32.
Kamati
ya Mashindano ya DRFA inaongozwa na Mwaisabula, wakati Makamu
Mwenyekiti ni Shaaban Mohamed huku wajumbe wakiwa ni Hugo Seseme, Daudi
Kanuti, Kassim Mustapha, Abeid Mziba na Bakari Mtumwa.
Imetolewa Novemba 26, 2013
Mohamed Mharizo
Ofisa Habari Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA).


0 comments:
Post a Comment