Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa
idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) kuhusu masuala
mbalimbali ya utendaji kazi wa idara hiyo. Kulia ni Naibu Waziri wa
wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil pamoja na Kamishna Mkuu wa
Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. Dk
Nchimbi aliwataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu. Mkutano huo
ulifanyika katika ofisi za Uhamiaji Makao Makuu, jijini Dar es Salaam
leo. (Picha na Felix Mwagara, Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).

Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na
watumishi wa Idara ya Uhamiaji Makao Makuu pamoja na wawakilishi wa
idara hiyo Mkoa wa Dar es Salaam. Dk Nchimbi alifanya
ziara ya siku moja katika Ofisi za Makao Makuu ya Idara hiyo, Kurasini
jijini Dar es Salaam leo kwa lengo la kuzungumza na watumishi hao
masuala mbalimbali ya utendaji kazi.. (Picha na Felix Mwagara, Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi).

Kamishna
wa Pasipoti na Uraia, wa Idara ya Uhamiaji, Victoria Lembeli (kushoto)
akimuuliza swali Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi
(wa pili kutoka kulia) kuhusu masuala mbalimbali ya maendeleo ya idara
hiyo. Watumishi mbalimbali waliuliza maswali pamoja na kutoa maoni yao
katika mkutano huo uliofanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya idara
hiyo, Kurasini jijini Dar es Salaam leo. Kulia
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. Kushoto (Meza Kuu)
ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil
pamoja na Kamishna Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Sylvester Ambokile Mwakinyule. (Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.).
KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
0 comments:
Post a Comment