Na Eleuteri Mangi-Maelezo
TAASISI
ya walemavu inayojishughulisha na masuala ya kisheria katika maendeleo
ya kijamii na kiuchumi ya watu wenye ulemavu (Dolased) imeanzisha mradi
wa kuinua ufahamu, kukuza na kulinda haki za kisheria za watu wenye
ulemavu na wasio na ulemavu ili akuhakikisha upatikanaji wa haki zao.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Dolased Gidion
Mandesi alipokuwa akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es
Salaam.
Mradi
huu wa Dolased unaongozwa na malengo yaliyoainishwa kwa nia ya
kufanikisha utoaji huduma kwa wahitaji hususani masuala ya kisheria.
“Taasisi
yangu itaenelea kutoa ushawishi na mbinu za kisheria katika utekelezaji
wa haki za watu wenye ulemavu na kuijengea uelewa jamii juu ya yaliyomo
kwenye sheria namba tisa ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2010 pamoja na
kanuni zake za mwaka 2012” alisema Mandesi.
Vivyo
hivyo Mandesi alisema kuwa malengo mahususi ya kufanikisha mradi wa
tasisi hiyo ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa haki kwa watu wenye
ulemavu na wasio na ulemavu nchini, kutoa mafunzo yz kisheria, kuratibu
na kuwachangamanish wasidizi wa kisheria wenye ulemavu katika wilaya
zenye vituo vya wasaidizi wa kisheria.
“Malengo
haya ni muhimu katika taasisi, dira yetu ni kuwa na jamii yenye kiwango
cha juu cha maendeleo endelevu kijamii ambapo haki za watu wenye
ulemavu zinazigatiwa na zinaheshimiwa” alisema Mandesi.
Mandesi
aliendelea kusema “Dhamira yetu ni kujikita na kujitolea katika
kuimarisha maisha ya watu wenye ulemavu, watoto, vijana na wazee kwa
kuzingatia mtazamo wa kijinsia nchini kwa kutumia mikakati
tuliojiwekea”.
Mikakati
inayosimamiwa na Dolased ni pamoja na kuimarisha mabadiliko ya kisheria
na kisheria, kuwajengea uelewa watu wenye ulemavu juu ya masuala
kisheria na haki za binadamu na kuwawezesha kiuchumi.
Mingine
ni kufanya tafiti, uchapishaji wa taarifa na usambazaji wa habari juu
ya hali za watu wenye ulemavu nchini na kuwashirikisha katika
ma[pambano dhidi ya ukimwi na virusi vya ukimwi pamoja na majanga
mengine.
Aidha,
Mandesi alisema kuwa zipo aina saba za ulemavu za ulemavu ambazo ni
wasioona, walemavu wa viungo, viziwi, albino, walmavu wa akili, wenye
uono hafifu na walemavu mchanganyiko.
Naye
kwa upande wake Afisa Mipango wa Taasisi ya Dolased Risala Msemo
alisema kuwa mradi huo utatekelezwa kwa kuwapa mafunzo kwa kuwajengea
uwezo watu wenye ulemavu 110 ili wawe na sifa za kuwa wasaidizi wa
msaada wa kisheria.
“Mafunzo
haya tutatoa katika kanda tatu ambazo ni kanda ya mashariki, kati na
kanda ya ziwa, mafunzo yatakuwa ya siku 25 ambayo yatagawanywa na
kutolewa kwa siku tano mfululizo yatakuwa ya awamu tano” ailsema Risala.
Risala
alisema kuwa taasisi hiyo imeandaa mwongozo sifa wawakilishi
watakaopata mafunzo na namna ya kuwapata walemavu watakaonufaika na
mafunzo hayo kutoka wilaya zote nchini.
Sifa
hizo ni pamoja na awe na elimu ya kanzia kidato cha nne na kuendelea na
kufaulu, awe mtu mwenye ulemavu, awe anatoka kwenye wilaya husika, awe
anamajina kamili matatu kwa ajili ya kumbukumbu na awe na umri wa miaka
18 na kuendelea.
Mradi huu unatekelezwa na Dolased katika mikoa ya Dar es Salaam ambayo ni makao makuu ya taasisi, Dodoma na Mwanza.
Tasisi
ya Dolased ilianzishwa Agosti 14, 1998 na mradi umeanzishwa na
kutekelezwa rasmi Agosti 1, 2013 na kufadhiliwa na Utoaji wa Msaada wa
kisheria (LSF) kwa muda wa miaka miwili na utakamilisha shughulu nzake
julai 31, 2015.
0 comments:
Post a Comment