Na Anna Nkinda – Maelezo, Lincoln
 Taasisi
 ya fursa ya  Elimu (Opportunity Education) ya nchini Marekani imeazimia
 kuanzisha mradi wa  laptop ndogo (tablets computer) kuanzia mwezi 
Januari mwaka 2014 nchini ambazo zitatumika kufundishia ili walimu 
waweze kufundisha haraka na kwa ufanisi zaidi pia wanafunzi watapata 
nafasi ya kujifunza  zaidi.
Hayo
 yamesemwa jana  na Joe Ricketts ambaye ni mwanzilishi na mtendaji mkuu 
wa taasisi hiyo wakati wa hafla ya kuchangia uugwaji mkono wa utoaji 
elimu barani Afrika iliyoandaliwa na taasisi ya Malaika  ya nchini humo 
na kufanyika katika  chuo Kikuu cha Nebraska kilichopo mjini Lincoln .
Ricketts
 alisema mradi huo kwa mara ya kwanza utaanzia nchini Tanzania ambapo 
wanafunzi zaidi ya 1000 kutoka shule 10 tofauti watapewa laptop ndogo 
kwa ajili ya kusomea na baada ya kipindi cha mwaka mmoja watafanya  
mtihani ili kuangalia tofauti iliyopo kwa wale waliokuwa wakitumia na 
wasiotumia. 
Baada
 ya majaribio hayo kama kutakuwa na mafanikio basi mradi huo utasambazwa
 katika shule nyingine nchini Tanzania ili kila mwanafunzi aweze kupata 
nafasi ya kusoma kwa kutumia laptop  hizo na hii itakuwa ni nafasi kwao 
ya kuweza kujitunza zaidi. 
“Kwa
 mara ya kwanza nilipokuwa nchini Tanzania nilipita  Serengeti na 
kukuta  mtu  anajitahidi  kutengeneza nyumba ambayo ni ngumu 
kuitengeneza hii inamaana kuwa mwalimu mmoja alikuwa anafundisha 
wanafunzi zaidi ya miamoja niliamua kuanzisha  mahusiano na shule hiyo 
ambayo niliwapelekea vifaa mbalimbali vya kufundishia”. 
“Lengo
 la  kuanzishwa kwa Taasisi hii ni kutoa msaada wa kielimu ikiwa na nia 
ya kufanya upatikanaji wa elimu bora kwa wanafunzi kutoka nchi 
zinazoendelea ili wale wanaotoka katika familia maskini waweze kusoma na
 kupata ajira pale watakapokuwa wamemaliza masomo yao na hivyo 
kujikwamua na hali ngumu ya maisha”, alisema Ricketts. 
Alimalizia
 kwa kusema kuwa program zao za kufundishia wanafunzi zimeandaliwa kwa 
lugha ya kiingreza lakini hivi sasa wameanza kuandaa program hizo kwa 
njia ya Kiswahili jambo ambalo litazifanya shule ambazo zinafundisha kwa
 lugha hiyo nazo kunufaika na Taasisi hiyo. 
Kwa
 upande wake Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliishukuru taasisi hiyo kwa
 kusaidia  kuboresha elimu nchini na kuiomba  kuangalia uwezekano wa 
kuzifikia  shule, walimu  na wanafunzi waliopo vijijini ambao nao 
wanahitaji kupata njenzo nzuri za kufundishia na material mazuri ya 
kusoma kama ilivyo kwa wanafunzi wa mjini.
Mama
 Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeeo 
(WAMA) alisema kuwa kupitia taasisi hiyo ameweza kuwasaidia watoto wa 
kike ambao ni yatima na wanaotoka katika mazingira hatarishi ambao 
hawakupata nafasi ya kupata elimu kuwapatia ufadhili wa masomo na hivyo 
kuendelea na masomo yao.
Pia
 ameweza kuinua uchumi wa wanawake jambo ambalo limewafanya waweze 
kuimarisha hali zao za maisha kwa kuwapatia elimu ya ujasiriamali na 
kuwaongezea mitaji ya vikundi vyao vya maendeleo.
Mama
 Kikwete alisema, “Nakupongeza Bwana Ricketts kwa kazi unayoifanya ya 
kuzisaidia shule zaidi ya 400 nchini Tanzania msaada unaoutoa wa vifaa 
vya kufundishia unawafanya walimu waweze kufundisha masomo yao vizuri 
naamini tutajenga mahusiano mazuri kati ya Taasisi yako na WAMA ili 
kuhakikisha kuwa program hii inafanikiwa na kutimiza malengo yake”.
Taasisi
 hiyo ilianzishwa mwaka 2005 na kusajiliwa nchini mwaka 2006 walianza 
kufanya kazi na shule moja ya msingi na hadi kufikia sasa  shule 434 
zikiwemo za Sekondari 33 zimenufaika kwa kupata vitabu, DVD na zana za 
kufundishia.
Kwa
 upande wa shule za sekondari wanatoa mwongozo wa mwalimu ambao 
unamuongoza kirahisi jinsi ya kuwafundisha wanafunzi , laptop ambazo 
zinamasomo yaliyorekodiwa ambayo ni ya sayansi, hesabu, kiingereza na 
maarifa ya jamii ,projecta na Televisheni ambazo zinasaidia kuonyesha 
masomo na vitabu na video inawasaidia wanafunzi kujifunza somo la 
kiingereza kwa njia ya kusikiliza na kusoma.
Mama
 Kikwete alipata nafasi ya kutembelea makao makuu ya Taasisi hiyo 
yaliyopo  katika mji wa Omaha na kujionea nyenzo mbalimbali za 
kufundishia vikiwemo vitabu na  DVD  zikiwa zimefungwa kwa ajili ya 
kupelekwa katika nchi mbalimbali zinazoendelea za bara la Afrika na Asia
 ikiwemo Tanzania.


0 comments:
Post a Comment