NA MAGRETH KINABO –MAELEZO
SERIKALI
imesema kwamba haijawafukuza wakimbizi nchini huku akitoa ufafanuzi
kuwa zoezi linaloendelea hivi sasa ni linahusiana kuwabaini na
kuwarejesha kwao wahamiaji haramu ambao wamekuwa wakiishi hapa nchini
kinyume cha sheria.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya
Ndani, Isaac Nantanga kufuatia vya habari vya nje ya nchi kutangaza
kuwa Serikali ya Tanzania imewarudisha kwao kwa nguvu wakimbizi 25,000
kutoka nchi ya Burundi katika kipindi cha muda wa mwezi mmoja uliopita.
“
Hakuna mkimbizi yeyote aliyerudishwa Burundi ,kwa hiari wala kwa nguvu
katika kipindi kilichotajwa. Kipindi cha mwisho cha kuwarejesha
wakimbizi kwa hiari kilikuwa mwaka 2012,ambapo hadi Desemba mwaka huo
wakimbizi 34,000 kutoka Burundi waliokuwa katika kambi ya Mtabila,
iliyoko Kigoma walirejeshwa makwao kwa hiari kwa ushirikiano wa
Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia
wakimbizi(UNHCR) na Serikali ya Burundi,” alisema Nantanga.
Alisema
Serikali Tanzania bado inaendelea kuwapa hifadhi wakimbizi kuendelea
kuishi kwenye kambi na makazi yaliyopo hapa nchini, ambapo jumla ya
wakimbizi 264,000 wanapata hifadhi.
“Hadi
leo wapo wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ( DRC) wapatao
64,172 kwenye kambi ya Nyarugusu iliyopo wilayani Kasulu, wakimbizi
175,473 kutoka Burundi wapo kwenye makazi ya wakimbizi ya Mishamo na
Katumba wilayani, mkoa wa Katavi na Bulyankulu mkoani Tabora.
Pia
wamo wakimbizi 2,128 kutoka Somalia kwenye makazi ya Chogo wilayani
Handeni,Tanga, wakimbizi 22,227 kwenye wilaya ya Kasulu na Kigoma
vijijini.
Taarifa
hiyo ilifafanua kwamba vyombo zoezi la kuwarudisha wahamiaji hao
lilianza Agosti mwaka huu. Lakini kabla ya hapo walipewa muda wa wiki
mbili kurejea kwao kwa hiari ama kupata vibali halali vya kuwawezesha
kuendelea kuishi hapa nchini.
“Hadi
Septemba 4, mwaka huu zaidi wahamiaji haramu 27,000 walikuwa wamerejea
kwao kwa hiari. Wahamiaji hawa haramu walikuwa katika mikoa ya Kagera,
Kigoma na Rukwa.
Baada
ya muda waliopewa wa kuondoka au kujisajili kihalali kuisha, Serikali
sasa imeaanza operesheni ya kuwabaini wahamiaji hao waliokaidi wito wa
kuwataka kuondoka kwa hiari ,” alisema Nantanga.
Nantanga
aliongeza kuwa operesheni hiyo inafanywa kwa uangalifu mkubwa ili
kuhakikisha kuwa wanaokamatwa na kurejeshwa kwao ni wahamiaji haramu
kweli na sio raia au wageni wenye hati halali za kuishi hapa nchini.
Aidha
alisema Serikali inatoa wito kwa vyombo vya habari vya ndani na nje ya
nchi kushirikiana na Serikali kutoa taarifa sahihi kwa kuwasiliana na
mamlaka husika pale wanapopelekewa taarifa zenye utata.
0 comments:
Post a Comment