


(Picha zote na Kibada Kibada Ofisi ya H/Wilaya ya Mpanda Katavi)
……………
Na Kibada Kibada –Mpanda Katavi
Wilaya
ya Mpanda Mkoa wa Katavi imetangaza oparasheni maalum ya kuwaondoa
wahamiaji holela waliovamia maeneo ya wazi ya mistu iliyotengwa na
serikali kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na kuharibu vyanzo vya maji
ya Mto Katuma ambao ndio tegemeo la wakazi wa Mji wa Mpanda kupata maji
ambayo pia yanategemewa na wanyama walioko hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Akizungumza
ofisini kwake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya
Mpanda ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Paza Mwamlima ameeleza
kuwa operation hiyo ni kwa ajili ya kuokoa uharibifu wa Mazingira na
Vyanzo vya maji hususani kuokoa uharibifu unaofanywa na watu waliovamia
maeneo ambayo hayaruhusiwi na kuweka makazi na kufanya shughuli zao za
uzalishaji mali hali ambayo inachangia uharibifu mkubwa wa mazingira.
Mkuu
huyo wa Wilaya ameeleza kuwa wageni wengi wanaoingia katika Wilaya ya
Mpanda wameathiri ardhi kutokana na mwingiliano wa wageni hao,sababu
nyingine zinazochangia uharibifu huo ni kuingia kwa mifugo kwa wingi
bila kufuata utaratibu hivyo kuchangia uharibifu wa mazingira hasa
wafugaji na wakulima wanaolima kandokando ya mto Katuma ambao
unategemewa na wananchi Mkoa wa Katavi hususani Wakazi wa Mji wa Mpanda
pamoja na hifadhi ya Taifa ya wanyama pori Katavi.
Hivyo
kutokana na mwingiliano huo ambao umeathiri sana mbuga hiyo ya Katavi
na wanyama kama viboko wanaoishi kwa kutegemea maji wanatabika na
wengine wanakufa kutokana na kukauka kwa maji ya Mto Katuma ambao
unamwaga maji yake katika Vijito vinavyotirirsha maji katika hifadhi
hiyo ya Katavi.
Kutokana
na hali hiyo ipo haja ya kupambana vya kutosha kulinda mto huo na
vyanzo vayke, hivyo inatakiwa kutoa elimu kwa wakulima na watu wanaolima
ovyo kwenye vyanzo vya maji,na pili kuwaondoa wale wote ambao
hawaruhusiwi kuishi maeneo ambayo hayakurusiwa hivyo ni wahamiaji holela
wanatakiwa wakakae kwenye vijiji vilivyopimwa.
Mkuu
huyo wa Wilaya ameyataja maeneo yatakayohusika na operasheni hiyo
itakayo anza Septemba 14,mwaka huu kuwa ni Eneo la Kamama lililopo
katika ya Makazi ya wakimbizi ya Mishamo naKata ya Mpandandogo,eneo
hili alieleza kuwa ni eneo la wazi kwa ajili ya matumizi ya Serikali.
Ameeleza
kuwa zipo hekta 46,000 zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za
Kiserikali ikiwemo shughuli za uwekezaji,pia limetengwa kwa ajili ya
shughuli za vijana wanaounda vikundi kwa kujiunga pamoja kwa ajili ya
shughuliza kilimo na uzalishaji mali, pamoja na eneo lingine
litakalotumika kwa ajili kwa kuweka Kambi ya Jeshi la kujenga Taifa JKT
Mkoani humo ambalo uongozi wa Mkoa uliomba upatiwe eneo hilo.
Eneo
la pili lililoathiriwa ni Mto Katuma ambalo limeathiriwa sana watu
wanolima hadi pembeni ya Mto,hivyo kuanzia Msimu ujao wananchi
wameelimishwa na kuellekezwa kuwa msimu wa kilimo ukifika watatakiwa
walime kuanzia mita 60 kando ya Mto ili kulindamazingira nakuepuka
uharibifu wa mazingira ili kuepuka kukausha maji ya Mto Katuma .
Akizungumzia
operasheni hiyo ameleza kuwa nyingine itanza Septemba 20 mwaka huu kwa
kuwapa elimu wananchi na wanaolima na kuishi kandokando ya Mto Katuma
kwa kuanza na hatua ya kuwaelimisha kuhusiana na madhara ya uharibifu
wa mazingira.
Pia
kuwa ameleza itafuatia na operation nyingine ya kuwahamisha wananchi
wanaoishi kwenye vilima vya Bugwe ambavyo ndiyo chanzo cha maji ya
vijito vyote vinavyotiririsha na kumwaga maji katika mto katuma.
Ameleza
kuwa vyanzo vyote vya mto luega, Katuma na na mito mingine vyanzo
vyake vya maji vinaanzia kwenye milima ya Bugwe kilipo kijiji cha Bugwe
na watu waliovamia bila utaratibu hasa kwenye milima ya Bugwe
wanatakiwa kuondoka na kurudi kijijini wakati taratibu zinafanyika
kuwaondoa na namna ya kukihamisha kijiji kwa kufuata taratibu kuhamisha.
Suala
la kijiji au kukifuta Kijij hicho liko nchini ya ofisi ya Waziri Mkuu
(TAMISEMI) wanaenedelea kuwasiliana na kuona namna ya kufanya.
Pamoja
na operasheni hiyo Mkuu wa Wilaya ameonya watakaohusika na operationi
hiyo kuzingatia taratibu kanuni na sheria bila kukiuka utaratibu akaonya
kuwa wafanye kazi kwa kufuata utaalamu na siyo kwa shuruti.
Kwanza
watoe elimu waweleze kwa nini wanataka kuwahamisha na pia washirikishe
viongozi wa serikali ya kijiji Wataalam wa maeneo husika ili kuondoa
migangano pamoja wanasiasa husika katika maeneo husika wala wasionee
mtu.
Akasisitiza kuwa sheria izingatie utu,izingatie utaratibu na ufuatwe na siyo kuathiri wala kukiuka haki za binadamu.
“Twende
kuelimisha kwanza na kuhamasisha”Naagiza mkafanye kazi kwa utaratibu
siyo shuruti wapewe elimu kwanini wanahamishwa.”alisema Mkuu wa Wilaya.
Kwa
Upande wake Kaimu Afisa Maliasili Mistu na Mazingira Josephin Rupia
alieleza kuwa kabla ya kuamua kufanya operasheni hiyo wameisha toa elimu
kwa wananchi na kutoa matangazo kuwa watu wanatakiwa kuondoka kwa hiali
kurudi vijijini maeneo yaliyopimwa.
Amesema
tayari viwanja zaidi ya miambili (200) kwa ajili ya makazi ya watu
vimepimwa katika Kijiji cha Vikonge hivyo mahali pa kuishi wameisha
tegewa hakuna haja kuendelea kuishi maeneo ambayo siyo rasmi na
hayaruhusiwi
0 comments:
Post a Comment