Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Sixtus Mapunda, akihutubia mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika kwenye Viwanja vya Komba Wapya, mjini Zanzibar, jana, baada ya mkutano wa Baraza Kuu la Jumuia hiyo kumalizika katika ukumbi wa Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui. Kushoto ni Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma. Watu waliohudhuria mkutano wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar wakishangilia. Mmoja wa mashabiki wa CCM aliyehudhuria mkutano wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar, akishangilia. Baadhi ya wananchi wakiwa wamepanda juu ya jengo kushuhudia kila kilichokuwa kikifanyika kwenye mkutano wa hadhara wa UVCCM uliofanyika Viwanja vya Komba Wapya, Zanzibar. Baadhi ya viongozi wa CCM, waliohudhuria mkutano wa hadhara wa UVCCM kwenye viwanja vya Komba Wapya mjini Zanzibar.
0 comments:
Post a Comment