Pichani: Mheshimiwa Dk. Migiro akiwa katika  picha ya pamoja na maafisa  wa
 Ubalozi. Kutoka kushoto ni Amos Msanjila, Allen Kuzilwa, Rose Henry 
Kiondo, Wema Kibona, Idris Zahran, Caroline Kitana Chipeta na Yusuf 
Kashangwa. 
Mjumbe
 wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama cha Mapinduzi 
(CCM) na Katibu wa NEC wa Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa 
Dk. Asha-Rose Migiro  atembelea Ubalozi wa Tanzania hapa London, kwa 
lengo la kuwasabahi maafisa wa Ubalozi na kuwapatia taarifa mbalimbali 
za maendeleo ya ushiirikiano na vyama marafiki na CCM, hususan Chama cha
 Labour cha Uingereza.
Mhe.
 Dk. Migiro alipita Ubalozini akitokea mji wa Brighton,  Kusini mwa 
Uingereza alikokuwa akihudhuria Mkutano Mkuu wa wa Chama cha Labour 
uliofanyika huko kuanzia tarehe 22 hadi 25 Septemba 2013. Katika 
mazungumzo yake na maafisa  hao Dk. Migiro aliwadokeza   kuwa akiwa 
Brighton alifanikiwa kukutana na kuanzisha mawasiliano na maafisa 
mbalimbali wa Chama cha Labour kwa lengo la kuimarisha zaidi ushirikiano
 wa vyama vyao.   


0 comments:
Post a Comment