Na Evelyn Mkokoi & Rashda Rashid
Ili
kufanikisha utekelezaji wa mkataba wa Montreal, serikali imeandaa na
kutekeleza programu ya Taifa ya kuondosha matumizi ya kemikali haribifu
kwa tabaka la ozoni. Akiongea kwa Niabaya ya waziri wanchi Ofisi ya
Makamu wa Rais Mazingira waziri mwenye dhamana ya kushughulikia masuala
ya Muungano Mh. Samia Hassan Suluhu alipozungumza na waandishi wa habari
ofisini kwake leo, amesema mikakati ya kitaifa ndani ya Programu hii ni
pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazosimamia utekelezaji wa
mkataba. , kutoa elimu kwa wadau na umma wa watanzania kuhusu umuhimu
wa Tabaka la Ozoni na hatari zinazolikabili,
Mheshimiwa
suluhu aliongeza kwa kusema kuwa kubadilisha technolojia katika viwanda
vinavyotumia kemikali haribifu na kutoa mafunzo yanayolenga kuimarisha
ujuzi katika sekta ya kuhudumia viyoyozi na majokofu na kuhamasisha na
kuhimiza matumizi ya kemikali na technolojia mbadala na rafiki kwa
tabaka la Ozoni ni njia ambazo serikali inatumia kunusuru kuharibika kwa
tabaka la hewa ya Ozoni
“Ni
muhimu tuzingatie kwamba juhudi za kila mmoja wetu zinatakiwa kupunguza
na kuondosha mathara katika Tabaka la Ozoni yanayo sababishwa na bidhaa
tunazo nunua na kutumia majumbani au sehemu za biashara alisisitiza.”
Mh
Suluhu aliwaasa wananchi kushiriki katika kuhifadhi Tabaka la Ozoni kwa
kuzingatia kuepuka kuingiza nchini gesi zilizopigwa marufuku, kuepuka
kutupa ovyo majokofu na viyoyozi chakavu ama vifaa vya kuzuia moto
vyenye kemikali zinazomong’onyoa tabaka la Ozoni,
Alitoa
wito kwa mafundi wa majokofu na viyoyozi waakikishe kuwa wananasa kwa
kutumia tena vipoozi (refrigerants) kutoka kwenye viyoyozi, na majokofu
wanayo hudumia badala ya kuviachia huru ili visisambae angani na
amewashauri mafundi hao watoe elimu kwa wateja wao juu ya njia raisi za
kutambua uvujaji wa vipoozi.
Maadhimisho
hayo ya siku ya Ozoni duniani ambayo huadhimishwa tarehe 19 ya mwezi wa
September kila mwaka, mwaka huu yatafanyika katika chuo cha
VETA-Nyakato jijini Mwanza yakiambatana na maonyesho ya bidhaa na
technolojia mbadala na rafiki kwa Tabaka la Ozoni Pamoja na mafunzo na
njia bora za technologia sahahi ya kuuudumia viyoyozi, majokofu na
mitambo ya kupoozea viwandani
Walengwa
wakubwa wa maadhimisho haya ni mafundi wa kuudumia majokofu viyoyozi
mitambo ya kupoozea kutoka viwandani vya kusindika minofu ya samaki
vinywaji na taasisi za ufundi zenye fani ya kuudumia majokofu na
viyoyozi. Lengo kuu ni kuelimisha mafundi kuhusu technolojia mpya.
0 comments:
Post a Comment