Friday, September 13, 2013

MJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI TANZANIA
 
Anuani ya Simu “MKUUPOLISI”                  
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                             Ofisi ya  Inspekta  Jenerali wa Polisi,
Simu : (022) 2110734                                                                                             Makao Makuu ya Polisi,
Fax Na. (022) 2135556                                                                                                          S.L.P. 9141,
Unapojibu tafadhali taja:                                                                                    DAR ES SALAAM.
 
                                                                             13 Septemba, 2013
 
TAARIFA YA JESHI LA POLISI KWA VYOMBO VYA HABARI
 
Tanzania imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika katika utekelezaji wa maazimio ya kikao cha 21 cha wakuu wa polisi Afrika  kilichofanyika Gaborone Botswana mwaka 2011, katika kuzuia na kutanzua makosa yanayovuka mipaka (Transitional Cross Border crimes).
 
Hayo yameelezwa katika kikao cha 22 cha  wakuu wa polisi kutoka nchi za Afrika (Interpol African Reginal Conference) kilichofanyika nchini Algeria kuanzia tarehe 10-12 Septemba, 2013.
 
Miongoni mwa makosa yaliyofanikiwa kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa na Jeshi la Polisi kupitia interpol Tanzania na kuiletea sifa nchi ya Tanzania, ambayo yamekuwa yakivuka mipaka ni pamoja na  ugaidi, uharamia, usafirishaji haramu wa binadamu, uzagaaji wa silaha ndogondogo, usafirishaji wa madawa ya kulevya na uingizaji wa dawa bandia.
 
Mbali na azimio hilo, maazimio mengine yaliyokuwa yameafikiwa kutekelezwa yalikuwa ni kuhakikisha kila nchi mwanachama wa interpol anajiunga katika mtambo wa mawasiliano wa interpol, kushiriki oparesheni za pamoja zinazoandaliwa na nchi wanachama na kushiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo maafisa wa polisi kwa lengo la kupambana na uhalifu, ambayo pia Jeshi la Polisi Tanzania limefanikiwa kuyatekeleza.
Imetolewa na:-
Advera Senso- SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video