Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hatimaye mshambuliaji wa Manchester United, raia wa Uholanzi, Robin van Persie amevunja ukimya na kutaka mshambuliaji mwenzake Wayne Mark Rooney kubakia na mabingwa hao wa ligi kuu nchini England
Rooney raia wa England hatima yake ya baadaye imekuwa matatani tangu meneja wake wa zamani Sir Alex Ferguson alipotangaza mnamo mwezi mei mwaka huu kuwa nyota huyo ameomba kuondoka
Suala la Rooney katika miezi mitatu ya kocha David Moyes tangu arithi mikoba ya Fergie, bado ni tete na leo hii ataikosha mechi ya ngao ya hisani dhidi ya Wigan.


Lakini Mholanzi huyo bado anaaminiRooney anao uwezo mkubwa sana wa kufanya kazi licha ya kutokea kwa matatizo.
ARV ameliambia gazeti la Sun: “Kila mtu anamtaka Wayne na nafikiri hata yeye anawaza hilo”
‘Moja ya sababu iliyonifanya nijiunge na Manchester United ilikuwa kucheza na Wayne.
‘Natumai atabakia hapa. Si kuwa ni mfungaji mzuri tu wa magoli, pia anafanya kazi kubwa akiwa uwanjani kuisaidia timu”.

0 comments:
Post a Comment