

Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini (UNIC) kwa kushirkiana na Soma Book Café walihamasisha kuanzishwa kwa Klabu za Kujisomea katika shule tatu za msingi ambazo ni Hananasif, Kumbukumbu na Oysterbay ili kujenga tabia ya kujisomea kwa watoto tangu utotoni. Klabu ya Kujisomea ya Shule ya Msingi Oysterbay imezinduliwa rasmi jana tarehe 31 Julai 2013 kwa kukabidhiwa mashelfu na vitabu vilivyotolewa na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Soma Book Café pamoja na Book Aid International kupitia Maktaba Kuu ya Taifa.



0 comments:
Post a Comment