Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard amekiri kuwa endapo mshambuliaji nyota wa klabu hiyo, Luis Suarez ataruhusiwa kuondoka majira haya ya kiangazi, suala hilo litaigharimu klabu na kuirudisha nyuma zaidi
Kiungo huyo raia wa England amemuelezea Suarez aliyekuwa kinara Anfield kwa kupachika mabao msimu uliopita kuwa ni mchezaji bora kuliko wote aliowahi kucheza nao na anatamani kuona nyota huyo raia wa Uruguay anabakia kwa majogoo wa jiji licha ya Real Madrid na wapinzani wao wa ligi kuu England, klabu ya Arsenal kumuwania.
Gerrard ameliambia gazeti la Daily Telegraph kuwa klabu haitakiwi kumuachia kirahisi mchezaji huyo mwenye ubora na kasi kubwa katika safu ya ushambuliaji, kwani itakuwa ngumu sana kumtafuta mchezaji kama huyo kucheza nafasi ya ushambuliaji msimu ujao.

Gerrard aliongeza kuwa nyota Wayne Rooney, Paul Scholes, Frank Lampard ni wachezaji wa kiwango cha juu. John Terry na Rio Ferdinand wapo nyuma yao kwa ubora. Lakini Suarez anatoka sayari nyingine na ni bora zaidi ya wote.
Pia Gerrard amemtaka Suarez kutokwenda Emirates licha ya kuwa atacheza ligi ya mabingwa barani Ulaya akiwa na Asernal.
The Gnners walishatuma ofa ya pauni milioni 41 wiki iliyopita, lakini ilikataliwa.


0 comments:
Post a Comment