Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
KOCHA wa Chelsea, Mreno Jose Mourinho amesema atapigana kufa na kupona mpaka siku ya mwisho katika jaribio lake la kumsajili mshambuliaji wa Manchster United, Wayne Mark Rooney majira haya ya kiangazi.
Chelsea yenye makazi yake darajani , jijini London, tayari walishatuma ofa mbili ambazo zimekataliwa na Manchester United, ofa ya mwisho inayotajwa kuwa ni zaidi ya paundi million 25 ilitumwa jumapili. Lakini Mourinho alisema: “Hatuna kizuizi cha muda kwenye suala hili.
‘Tumemuona Rooney ni mchezaji ambaye tungependa kuwa nae. Tumefanya kila kitu kwa utaratibu unaopaswa na tutafanya hivyo mpaka siku ya mwisho ya usajili”. Alisema Mourinho.
Rooney inaaminika kwamba amemwambia kocha wake David Moyes kwamba anataka kuondoka, lakini United imekuwa ikisisitiza kwamba hauzwi.



Wakati huo huo mbio za Manchester United kuiwania saini ya kiungo mahiri wa FC Barcelona, Cesc Fabregas zinaonekana kufikia ukingoni baada ya nyota huyo kusema anatamani kuendelea kufanya kazi Nou Camp.
Fabregas alisema: ‘Makombe ya Barcelon ndio kitu ambacho nimekuwa nikitumainia katika maisha yangu, imekuwa ndoto yangu toka enzi za utoto wangu. Sijazungumza na klabu yoyote kwa miaka miwili iliyopita”

0 comments:
Post a Comment