Na Baraka Mpenja
Viongozi
wa maafande wa Tanzania Prisons ya jijini Mbeya maarufu kwa jina la
“Wajelajela” wamekiri kumalizana na kiungo mahiri wa klabu ya Yanga ya
Dar es salaam, Omega Seme ambaye anajiunga kwa mkopo na timu yake ya
zamani.
Katibu
mkuu wa wajelajela, Sadick Jumbe amewashukuru viongozi wa Yanga
kuwaelewa na kuwaruhusu kumchukua mchezaji huyo, na julai 5 siku ya
Ijumaa atakuwepo jijini Mbeya kujiunga na wenzake.
Jumbe
alisema msema kweli ni mpenzi wa mungu, Yanga wamewapa kwa mkopo na sio
kwamba wamemnunua, kikubwa alisisitiza kuwa nyota huyo alianzia soka
Prisons na sasa amerejea nyumbani ambapo wanaamini watafanya makubwa
akiwepo kikosini.
“Omega
ni kijana mzuri, anacheza vizuri sana. Anahimili sana safu ya kiungo,
tumepata mkataba wake na tunajua atafanya vizuri sana akicheza namba
nane”. Alisema Jumbe.
Pia
katibu huyo alisema kinda huyo alikuwa miongoni mwa majina ambayo kocha
wao mkuu Jumanne Chale alipendekeza, hivyo Yanga kuwapatia kijana huyo
wanashukuru sana.
Kwa
upande wake Omega seme, alisema mpaka sasa hawezi kusema lolote, lakini
siku ya Ijumaa atazungumza na kuweka wazi suala lake.
“Kila kitu namaliza Ijumaa, unajua unapopelekwa kwa mkopo unaweza kukubali au kukataa”. Alisema Omega.
Akizungumzia
kuondokewa na baadhi ya wachezaji wao akiwemo Sino Agostino aliyetimkia
kunako klabu ya Msimbazi, kipa David Abdallah aliyehamia Mbeya City,
Elias Maguli aliyejiunga na Ruvu Shooting, katibu huyo alisema wamepata
nyota wapya walioziba nafasi za wachezaji hao.
“Tuna wachezaji wengi sana, Enock Nyanda, Madafa, Ibrahim saka na wengine wengi, wanaotosha kuziba nafasi zao”. Alisema Jumbe.
Pia
alisisitiza kuwa msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara watakuwa fiti
mno, watatoa upinzania mkubwa sana na kuwashangaza wanaojiita wafalme wa
soka la Tanzania, Yanga na Simba.
Jumbe
alisema jina la Prisons sio geni masikioni mwa watu, ni timu yenye
historia ya kufanya vizuri sana, sasa timu ile iliyowakilisha taifa
michuano ya kimataifa ipo njiani.
“Nimeweka
muziki mkali, siku nitakayokuja kucheza na Simba au Yanga Dar es
salaam, tafadhali mashabiki waje waone makali yetu, tutakufa na mtu”.
Alisema Jumbe.
0 comments:
Post a Comment