Saturday, July 20, 2013


SONY DSCNa Baraka Mpenja 
Mabingwa wa soka Tanzania bara, klabu ya Yanga chini ya kocha mzungu, Mholanzi Ernie Brandts akisaidiana na kocha mzawa Fred Ferlix Minziro wamewataka mashabiki wao na mashabiki wa timu pinzani wakiwemo watani wao wa jadi, Simba, kujitokeza kwa wingi katika mchezo wa kesho wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wakusanya mapato wa Uganda, klabu ya URA, katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam.
Yanga waliokuwa ziarani katika mikoa ya Kanda ya ziwa na hatimaye kwenda mkoani Tabora ambako walicheza mechi tatu za kirafiki na kushindwa kupata ushindi katika mechi zote, kwa maana ya kutoka suluhu moja, sare ya 1-1 na kufungwa 2-1, watashukam dimbani ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya ligi kuu Tanzania bara na mashindano ya klabu bingwa barani Afrika.
Afisa habari wa klabu hiyo, Baraka Kizuguto ameiambia MATUKIO DUNIANI kuwa vijana wapo safi, morali yao ipo juu na jana walifanya mazoezi, lakini leo watafanya mazoezi ya mwisho kujiandaa na kipute cha kesho.
“Yanga ni timu bora zaidi kwa sasa, ina wachezaji wazuri wanaojua kucheza soka la kitabuni, njooni muone vijana wa jangwani wanavyopiga soka safi hapo kesho mbele ya URA ya Uganda”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema kutokana na ubora wa URA, itakuwa nafasi nzuri kwa wachezaji wa Yanga kujipima ubavu huku mwalimu Brandts akiangalia uwezo wa wanandinga wake wapya waliowasajili kwa ajili ya ligi kuu na michuano ya kimataifa.
“Itakuwa mechi nzuri sana kwetu, kocha sio mtu wa maneno sana, nadhani wengi mnafahamu, lakini kwa upande wake anaendelea na mazoezi kwa umakini mkubwa kwani kushinda mechi kubwa ya kimataifa inajenga imani kubwa kwa wachezaji na mashabiki wa timu, hivyo itatumia wachezaji wote wapya kuangalia uwezo wao”. Alisema Kizuguto.
Afisa habari huyo alisisitiza kuwa Yanga kwa sasa anajipanga kutetea ubingwa wao walioutwaa msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa kwani wao ndio wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika.
“Ujue tuna majukumu mengi sana kwa msimu ujao, kwanza kulinda ubingwa wetu, tunajua watani zetu wanajipanga sana hasa ukikumbuka tulimaliza ligi kwa kuwafunga, wana hasira na sisi, tumesajili na kuongeza nguvu zaidi, hakika msimu ujao tutashinda mechi zote”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto aliwataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi hapo kesho kuishangilia timu yao kwani lazima ifanye vizuri kutokana na kikosi kusheheni nyota wenye ubora wa juu.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video