Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
“Hata wazee wa zamani walishasemaga kazi na dawa” . Baada ya shughuli pevu ya mazoezi ya kusukumu gozi la ng`ombe lazima upunge upepo kwanza bwana”. Chelsea wanatimiza sana wajibu wa afya, wamepiga mazoezi na kupunga upepo kwa kuogelea na kupiga stori za nje ya uwanja.
Wakati kocha mwenye mbwembwe nyingi Mreno, Jose Mourinho akisaini mkataba wa kurejea tena darajani kuwanoa matajiri wa London, klabuya Chelsea, alisisitiza kuwa kwa sasa anaitwa “The Happy One” kwa tafsiri isiyo rasmi “Mtu mwenye furaha” badala ya jina lake lililozoeleka la “The special One” kwa maana ya “Mtu Maalumu”.
Ukweli wa maneno yake umeonekana leo wakati akizungumza na waandishi wa habari Bangkok nchini Thailand, pia alipoenda na kikosi chake katika uwanja wa mazoezi.
Mourinho alionekana mwenye furaha ya kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani ambayo aliihama mnamo mwaka 2006 baada ya kutofautiaba na mmiliki wa timu hiyo Bilionea Roman Abramovich ambaye aliamua kumrudisha tena darajani.
Mourinho alipigwa picha leo jumatatu akizunguka na koni yake ya mazoezi kwa wachezaji wake katika uwanja wa shule ya Kimataifa ya Bangkok, nchini Thailand ambapo wapo katika ziara ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England.
Mourinho alionekana akipigwa jua katika uwanja huo wakati wachezaji wake wakifurahia maisha katika bwawa maridhawa la kuogegelea, ikiwa ni sehemu ya kujipoza shughuli za kutwa.
Baadhi ya wachezaji akiwemo Nahodha John Terry, Ashley Cole na Gary Cahil walionekana kufurahia zaidi maisha ya kuogelea na kupunga upepo.
Branislav Ivanovic, alionesha maujanja zaidi baada ya kuogelea kwa ufundi wa juu na kuwaonesha wenzake kuwa kazi yake sio kuzuia mipira tu akiwa uwanjani, bali hata kuogelea anajua sana.
Romelu Lukaku, aliyerudishwa kundini akitokea West Bromwich Albion msimu uliopita alikokuwa anacheza kwa mkopo, alitumia fursa hiyo kumkaribisha klabuni hapo mchezaji mwenzake mpya ambaye hakumkuta wakati akicheza kwa mkopo, Eden Hazard kwa kutumia njia ya kumnyunyizia maji mithiri ya bomba la kuogea maarufu kama shawa.
Akiwa kibaruani, hakuna masihara: Jose Mourinho akiwa na koni kwa ajili ya mazoezi ya wachezaji wake huku jua likiwaka nchini Thailand
Siku za furaha: Mourinho akicheka na mtu wake wa kazi (kulia) bwana Rui Faria wakiwa katika bwawa la kuogolea
Daah! ebwana maji si baridi sana: John Terry, Gary Cahill na Ashley Cole wakioga maji ya ubaridi baada ya mazoezi 
Mcheki maujanja: Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic akionesha ufundi wa kuogelea
Shwari sana: Nathaniel Chalobah akionekana mwenye furaha kubwa baada ya kurejea Chelsea kuendelea na kazi yake ya kusakata kabumbu
Mambo si ndio haya swahiba: Romelu Lukaku na Ryan Bertrand wakipunga upepo katika maisha yao ya ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu
Tulia mwanangu: Marco Van Ginkel, Ramires, Victor Moses, na Cole wakifurahia kuoga
Makinda : Kevin de Bruyne na Nathaniel Chalobah wakipunga upepo baada ya mazoezi, ama kweli kazi na dawaRATIBA YA MECHI ZA CHELSEA YA MAANDALIZI YA MECHI ZA MSIMU MPYA
July 17 Singha All-Stars (Rajamangala Stadium, Bangkok – Singha 80th Anniversary Cup) 2pm
July 21 Malaysia XI (Kuala Lumpur – BNI Cup 2013) 2.45pm
July 25 BNI Indonesia All-Stars (Gelora Bung Karno National Stadium, Jakarta) 2pm
August 2 Inter Milan (Lucas Oil Stadium, Indianapolis – Guinness International Champions Cup) 1am

Lowa lowa lowa: Eden Hazard akilowanishwa na Lukaku wakati wa kupunga upepo katika bwawa la kuogelea
Jembe jipya: Van Ginkel amekuwa akifananishwa na Justin Bieber… na mashabiki wake wa kike, walahi lazima wafurahie picha hii
Jembe jipya: Van Ginkel amekuwa akifananishwa na Justin Bieber… na mashabiki wake wa kike, walahi lazima wafurahie picha hii
Anaonesha kiwango cha juu: PSG wamevutiwa na Ivanovic wakitaka kumsajili kwa ada ya uhamisho ya pauni milioni 8
0 comments:
Post a Comment