Na Baraka Mpenja
Mabingwa
wa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara, klabu ya Yanga ya Dar es
salaam “kwalalumpa Malysia” kesho wanaanza kupasha misuli yao moto
kujiandaa na mitanange ya ligi kuu msimu wa 2013/2014 na michuano ya
ligi ya mabingwa barani Afrika.
Afisa habari wa klabu hiyo Baraka Kizuguto amezungumza na MATUKIO DUNIANI
na kubainisha kuwa Yanga wanaanza mazoezi na sio kambi hapo kesho
maeneo ya Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, iliyopo Mabibo, Dar es
Salaam.
“Ni
kweli kesho tunaanza mazoezi, kila kitu kinakwenda vizuri, na hapo
kesho tunaanza mazoezi. Naomba tuongee vizuri na si kupotoshana taarifa,
kesho Yanga inaanza mazoezi na sio kambi”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto
Alisema kwa siku kadhaa wachezaji watakuwa wakijifua na kurejea makwao,
kabla ya kuingia kambini rasmi zikisalia wiki chache kabla ya kuanza
kwa ligi.
Afisa
habari huyo alisisitiza kuwa kesho mazoezi yanaanza saa mbili asubuhi
ambapo kocha wao mkuu, Mholanzi ambaye anatarajia kuwasili leo kutoka
kwao, Ernie Brandts ataongoza mazoezi hayo.
“Mwalimu
atawasili leo na kesho atakuwepo mazoezini, kikubwa ni mashabiki wetu
kuwa na imani kubwa na vijana wao”. Alisema Kizuguto.
Afisa
habari huyo aliongeza kuwa wachezaji wote wanatambua juu ya kuanza
mazoezi hayo, hivyo kesho mapema asubuhi watakuwepo uwanjani kwa ajili
ya maandalizi ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara.
Mabingwa
hao ambao watakuwa wawakilishi pekee wa Tanzania katika michuano ya
ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani, wanaendelea na zoezi la usajili
pamoja na kuwaongezee mikataba baadhi ya wachezaji wao.
Leo
hii taarifa za ndani kutoka katika klabu hiyo zinaeleza kuwa wachezaji
nyota wa klabu hiyo Nizar Khalfan na Oscar Samwel Joshua wameongezewa
mikataba ya miaka miwili.
0 comments:
Post a Comment