Tuesday, July 23, 2013


12
Na Gladness  Mushi, Arusha
Nchi ya Tanzania inakabiliwa na changamoto kubwa  la pengo la uongozi hali ambayo  nchi ina rasilimali nyingi za utajiri lakini wananchi
wake wengi ni maskini  ambapo viongozi wengi wamepotezai ya uwajibikaji kwa wananchi wao.
Hayo yamesemwa na Naibu waziri wa maliasili na utalii  Mh.Lazaro Nyalandu kwenye mahafali ya nne ya chuo cha Habari maalum katika
hotuba yake  kwa wahitimu hao yaliyofanyika jana chuoni hapo eneo la ngaramtoni mkoani arusha
Hata hivyo alisema kuwa kumekuwepo baadhi ya viongozi kuwa na dhana ya  kutowajibika ipasavyo katika majukum yao hali ambayo inazidi kuongeza hali ya umaskini kwa wananchi walio wengi,na endapo viongozi wangewajibika ingesaidia kuongeza ufanisi katika kuleta maendeleo kwa wananchi nakupunguza umaskini na kuongeza tija na ufanisi zaidi.
Pia ameiasa jamii kuondoa dhana ya kudharau kitu ambacho mtu mwingine anafanya badala yake waungane kwa pamoja ili kuweza kuongeza tija na ufanisi zaidi na kuwa chachu ya maendeleo kwa taifa na bara la afrika.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo hicho cha Habari Maalumu Bw.Jackson Kaluzi alisema kuwa mbali ya mafanikio ya uanzishwaji wa chuo hicho kuwa msada mkubwa kwa wananchi wandani na bara la afrika lakini wamekuwa na changamoto kubwa  ya uhaba wa ardhi ambapo katika eneo hilo viwanja vimekuwa vikiuzwa kwa bei kubwa sana hali ambayo inawakwamisha kuweza kupanua majengo ili kuweza kuongeza wanafunzi wengi kutoka nchi mbalimbali.
Aidha katika mahafali hayo wamehtimu wanafunzi  12 kwa ngazi ya diploma katika masomo ya uongozi na utawala kutoka nchi mbalimbali za Bara la afrika ikiwemo Tanzania,Rwanda,Burundi ,Uganda ,Kenya na Drc kongo.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video