Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
“Mwaka huu ni sawa ni miaka mingine, Machester City itakuwa juu ya Manchester United. Tutajaribu angalau. Nilicheza na United mara mbili katika ligi ya mabingwa barani Ulaya nikiwa na Villarreal”.
“Katika miaka hiyo miwili tulifika hatua ya 16 bora na Man City hawakufanya hivyo”.
Sasa Shughuli ndio imeanza, maneno hayo hapo juu kaunguruma kochwa mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini akizungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza tangu ateuliwe kuwa kocha wa klabu hiyo.
Pellegrini alisema klabu yake itarejesha upinzani mkubwa kwa United na msimu ujao lazima wawapokonye ubingwa mashetani hao wekundu.
Akiwapasha wanahabari leo katika mkutano wake wa kwanza, Pellegrini alikumbusha historia ya kukutana na Sir Alex Ferguson mara nne katika ligi ya mabingwa barani Ulaya hatua ya makundi, kwa maana ya mara mbili mwaka 2005 na mara mbili 2009, na mashetani hao walishindwa kufunga hata bao moja katika suluhu hizo nne.
Bosi huyo alisema; `Najua kitu muhimu kwa mashabiki wote wa City ni kuwafunga Manchester United na kama nipo hapa ni kwa sababu nina uhakika wa kufanya hivyo.
Uso kwa uso na Kamera: Kocha mpya wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameitisha mkutano wake wa kwanza katika uwanja wake wa mazoezi leo hii
Pata T-shirt kijana: Mchezaji wa kwanza katika usajili wa Pellegrini ni nyota Fernandinho
Akilonga mbele ya mike: Pellegrini akijibu maswali katika mkutano na waandishi wa habari
Macho yote : Pellegrini aliitisha mkutano wa kwanza leo hii katika uwanja wa mazoezi tangu atambulishwe rasmi kuwa mrithi wa Roberto Mancini
Kabla ya kukutana na waaandishi: Pellegrini akijiandaa kuzungumza na waandishi wa habari kwa mara ya kwanza
Tayari kwenda: Pelligrini kabla ya kwenda katika mkutano na waandishi wa habari
Mpinzani mkubwa: Pellegrini atapimana ubavu na kocha wa United David Moyes 
0 comments:
Post a Comment