Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sporstmail.com
“Kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza”. Kuna baadhi ya wachezaji wanahaha kutafuta timu za kuchezea, wakati huo huo wengine wanabembelezwa kubakia kuzichezea timu zao ilihali wao wametangaza kuzihama.
Wakati suala la mshambuliaji wa Mabingwa wa ligi kuu soka nchini England na timu ya taifa ya nchi hiyo, Wayne Mark Rooney likizidi kutanda ukungu, leo hii kocha wake David Moyes amefichua kuwa amekutana katika mazungumzo na Ronney mara nne tangu ateuliwe kuwa kocha mpya baada ya Sir Alexndar Chapman Ferguson “Sir Ferguson” kustaafu, hivyo kila kitu kinaenda sawa na hataondoka klabuni hapo.
Ingawa Moyes hajathibitisha kama Rooney amesema wazi kuwa anabakia Old Trafford, lakini kocha huyo amesisistiza kuwa nyota huyo aliyeingia katika mgogoro na Sir Fergie , kamwe hataondoka klabuni hapo.
Mshambuliaji huyo, baba kwa watoto wawili kwa sasa, yumo katika orodha ya wachezaji 19 watakaokuwa ziarani na ratiba yao inaonesha wataenda Thailand, Australia, Japan na Hong Kong.
Wakati Moyes akisema hayo, matajiri wa London, Chelsea, wametangaza ofa ya pauni milioni 60 kumsajili Rooney na Mourinho amesema kuwa endapo nyota huyo atakubali kuihama United, watamlipa kiasi cha pauni laki mbili na elfu arobaini kwa wiki, pamoja na mkataba wa miaka mitano.
Moyes akiongea na talkSPORT amesema: ‘Timu imeshasema kuwa Wayne atabakia na hauzwi. Nimekutana naye mara mbili, tatu, nne na ndio maana kila siku yupo hapa. Nimekutana naye mara nyingi sana”.
Wayne alikuja nyumbani kwangu nami nimeenda nyumbani kwake na tukafanya mazungumzo. Anaendelea na mazoezi vizuri sana. Timu imesema kwa miaka mitano amekuwa katika kiwango kizuri na umbo moja, nami pia nimelichulia vizuri suala hilo.
“Tumeshasema hauzwi na nitajitahidi kurudisha Wayne Rooney wa ukweli kadri niwezavyo”. Alisema Moyes.


Wameungana: David Moyes na Wayne Rooney wakiondoka kwenda katika ziara yao ya maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu soka nchini England



Kamvutia : Moyes asema ana umbo zuri la kiuchezaji zaidi ya wachezaji wengi aliokaa nao
Kikosi cha United kilichoondoka kwenda Ziarani leo
Makipa: Anders Lindegaard, Ben Amos
Walinzi: Rafael, Phil Jones, Rio Ferdinand, Jonny Evans, Patrice Evra, Alex Buttner, Fabio, Michael Keane
Viungo: Michael Carrick, Anderson, Tom Cleverley, Ryan Giggs, Wilfried Zaha, Jesse Lingard, Adnan Januzaj
Washambuliaji: Wayne Rooney, Danny Welbeck
Robin van Persie na David de Gea watajiunga na kikosi Sydney.
Shinji Kagawa amepewa mapumziko na atajiunga na timu siku chache zijazo
Javier Hernandez ataikosa ziara hiyo kwani ametoka kuitumikia timu yake ya Taifa ya Mexico siku chache zilizopita katika mashindano ya kombe la Mabara.

0 comments:
Post a Comment