Muonekano
wa Banda la MeTL Group lililopo kwenye maonyesho ya 37 kimataifa ya
Biashara yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini
Dar es salaam.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiwa na Mkurugenzi wa Masoko na
Mauzo wa Makampuni ya MeTL Group Hussein Dewji wakati alipotembelea
Banda la Kampuni hiyo kwenye maonyesho ya 37 ya Biashara ya Kimataifa
yanayoendelea katika uwanja wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es
salaam.
Mstahiki
Meya Jerry Silaa akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo
wa Makampuni ya MeTL Group Bw. Hussein Dewji ambapo pia alimpongeza kwa
bidhaa nzuri wanazozalisha katika kampuni yao.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiendelea kuzungukia bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na Kampuni ya MeTL Group kwenye banda hilo.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akisalimiana na warembo wanaotoa huduma katika banda hilo ambao wamevalia Khanga zinazotengenezwa kiwanda cha 21 Century Textile cha MeTL .
Pichani
juu na Chini ni Wananchi wakimiminika kwenye Banda la kampuni ya MeTL
Group kujipatia mahitaji mbalimbali ya nyumbani zikiwemo Sabuni za
kufulia, Unga, Mafuta ya kupikia, Vitenge, Khanga na vingine vingi.


Baadhi
ya Kinamama wakisaidiwa kuchagua Khanga na Vitenge na mmoja wa warembo
nadhifu wa MeTL wanaotoa huduma kwa wateja katika banda hilo.
Bidhaa
mpya ya Kampuni ya MeTL Group “Sheeba Shake” yenye ladha tatu za
kuvutia ikiwemo Vanilla, Chocolate na Banana. Kinywaji hicho kitaingia
mtaani baada ya maonesho haya kumalizika. Kinatia nguvu na
kukuburudisha.




0 comments:
Post a Comment