Monday, July 15, 2013


Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Ikiwa ni mikakati wa kujiandaa na msimu mpwa wa ligi kuu soka Tanzania bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 24 mwaka huu, klabu za Azam fc na Ashanti United zinatarajia kushuka dimbani kuoneshana kazi hapo kesho uwanja wa Chamazi Mbande nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
Afisa habari wa Azam fc, Jafar Idd Maganga amethibitisha kuwepo kwa mechi hiyo na kudai kuwa itakuwa nafasi nzuri kwa benchi la ufundi kutazama uwezo wa wasukuma kabumbu wao baada ya mazoezi ya siku nyingi.
“Tutakabiliana na Ashanti hapa nyumbani, ni mchezo wa kirafiki wa kawaida, lakini ni muhimu kwa makocha wetu kupima uwezo wa kikosi chao, hivyo mashabiki waje waone mchezo huo”. Alisema Jafar.
8lambalamba1
Jafar aliongeza kuwa mazoezi yao yanaendelea vizuri, huku kocha mkuu Sterwart John Hall akiwa na mpango mzito wa kutwaa ubingwa msimu ujao.
“Malengo yetu ni kuhakikisha tunatwaa taji la ligi kuu msimu ujao, lakini ukumbuke kuwa kwa mara nyingine sisi ni wawakilishi wa Tanzania katika michunao ya kombe la shirikisho barani Afrika mwakani, hivyo maandalizi yetu yamelenga ligi kuu na michauno ya kimataifa”. Alisema Jafar.
Afisa habari huyo wa wana lambalamba alisisitiza kuwa toka awali walishatangaza kuwa Azam fc imekuja kuleta mapinduzi ya soka la Tanzania, na nia yao iko pale pale.
“Sisi tunafanya jitihada kubwa ya kuandaa kikosi bora cha mapinduzi ya soka la Tanzania na kuua ufalme wa Simba na Yanga, hakika kila kitu kitawezekana kutokana na mipango mizuri ya benchi la ufundi pamoja na viongozi wa klabu, cha msingi Watanzania watupe sapoti kubwa zaidi”. Alisema Jajar.
DSC_3806Wakati Azam fc wakisema hayo, nao Ashanti United waliotangaza kuwepo kwa mechi hiyo tangu wiki iliyopita, wamesema wamefurahi kukutana na washindi wa pili wa ligi kuu Tanzania bara kwa misimu miwili mfululizo.
Katibu mkuu wa Ashanti , Abubakar Sellasi aliimbia FULLSHANGWE kuwa wanajiandaa vizuri na msimu ujao wa ligi kuu kwani ndio kwanza utakuwa msimu wao mpya kabisa baada ya kutoka kucheza ligi daraja la kwanza msimu uliopita.
“Tunaendelea vizuri  na mazoezi ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji wazuri, lakini kesho tutakuwa na mechi ya kirafiki na Azam fc katika uwanja wao wa nyumbani wa Chamazi. Ni mechi nzuri kwetu kuangalia uwezo wa kikosi chetu, maandalizi yote yanakwenda barabara”. Alisema Sellasi.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video