Mke
wa Rais wa Marekani mama Michelle Barack Obama akiwasili katika ofisi za
Wanawake na Maendeleo WAMA jioni hii wakati alipotembelea katika ofisi
hiyo na kuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Mwenyekiti wa WAMA Mama
Salma Kikwete katika makao makuu ya taaisis hiyo leo, Rais Barack Obama
na Mke wake Michelle Obama wako katika ziara ya siku mbili ya kikazi
nchini Tanzania wakiongozana na watoto wao jioni hii Rais Barack Obama
atakuwa na mazungumzo na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete na pia
watazungumza na waandishi wa habari Ikulu kabla ya kuendelea na kazi
zingine.PICHA NA KIKOSI KAZI CHA FULLSHANGWE

Mama Michelle Obama akilakiwa na mwenyeji wake mama Salma Kikwete wakati alipowasili katika ofisi hizo kwa mazungumzo mafupi.

Mama
Anna Mkapa ambaye pia ni mwenyekiti wa taasisi ya EPTF akiongozana na
mama Aisha Bilal wakati wa mapokezi ya Mke wa Rais Barack Obama Mama
Michelle Obama katika ofisi za WAMA jioni hii

Mama
Salma Kikwete akiwapungia mkono wake wa Viongozi wakati alipowasili
katika ofisi za WAMA tayari kwa kumpokea mgeni wake Mama Michelle Obama.
0 comments:
Post a Comment