Thursday, July 11, 2013


e76dYanga1
Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam
Hatimaye ziara ya mikoani ya mabingwa wa kutandaza kabumbu Tanzania bara, Wanajangwani wanaovalia uzi wa njano na kijani, Dar Young Africans, inakamilika leo kwa kushuka ugani kupambana na maafande wa Rhino Rangers waliopanda kucheza ligi kuu msimu ujao katika mchezo wa kirafiki ndani ya uwanja wa Ally Hassan Mwinyi, mjini Tabora.
Akizungumza na mtandao wa FULLSHANGWE, Afisa habari wa Yanga waliobatizwa jina la “Wazee wa Uturuki, wazee wa Sambusa” msimu uliopita, Baraka Kizuguto amesema  awali walitakiwa kucheza na wakata miwa wa Mtibwa Sugar, lakini waratibu wa ziara yao wamebadilisha kwa madai kuwa kuna mambo hayakwenda sawa kwa waandaaji pamoja na makubaliano na watoto hao wa Manungu Turiani.
“Hali ya hewa ya Tabora ni shwari kabisa, wachezaji wapo salama, na jana tulifanya mazoezi kujiandaa na mechi dhidi ya wenyeji  wetu, ni fursa kubwa kwa mashabiki na wanachama wa Yanga wa mkoani Tabora kuitazama timu yao”. Alisema Kizuguto.
Kizuguto alisema licha ya kushindwa kutamba katika mechi mbili zilizopia dhidi ya Mabingwa wa Uganda, KCC, ambapo mchezo wa kwanza jijini Mwanza walitoka suluhu na kupoteza mechi ya marudiano katika uwanja wa Kambarage Mkoani Shinyanga,  leo hii watajitahidi kufa na kupona kuhakikisha wanaonesha soka safi na kuwaumsha mashabiki wao kwa shangwe, nderemo na vifijo.
“Ni kawaida ya Yanga kuonesha soka la kufundishika, sisi ni mabingwa, lazima tuoneshe uwezo mkubwa tunapokuwa uwanjani, mashabiki wa Tabora watafurahia mambo ya vijana wa Jangwani  leo hii”. Alisema Kizuguto.
Afisa habari huyo alisema mashabiki wa mkoani Tabora wamewaunga mkono kwa kiasi kibwa, huku akisema wamefanikiwa kuwaandikisha wanachama halali zaidi ya hamsini na kuwapa kadi za uanachama wa klabu.
“Hakika tumepata mafanikio kanda ya ziwa na hapa mkoani Tabora, tumepata wanachama wapya ambao tumewapatia kadi kabisa, haya ni matunda ya ziara yetu kiukweli”. Alitamba Kizuguto.
BRANDTS
Kocha wa Yanga, Ernie Brandts
Kizuguto aliongeza kuwa baada ya mechi hiyo, kikosi cha wana Jangwani kitaondoka mkoani Tabora kesho Ijumaa na kurejea Dar es salaam kuendelea na mipango mingine ya mazoezi.
Yanga baada ya kutwaa ubingwa msimu uliopita na kuwapokonya watani wao wa jadi, Simba SC, sasa wana kibarua kikubwa cha kuandaa timu kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika mwakani. Wenzao Simba wanaujua moto wake baada ya kutolewa nishai na Libolo ya Angola kwa kipigo cha nje ndani cha mabao 5-0.
Wakati hayo yakijili kwa Yanga, nao watani wao wa jadi, wekundu wa Msimbazi Simba walimaliza ziara yao mkoani Katavi jana jioni kwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Kombaini ya Katavi na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Mnyama yupo ziarani mkoani Katavi kwa mwaliko maalumu wa waziri mkuu, “Mtoto wa Mkulima”, mzawa wa katavi, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda.
Pia walishuka dimbani mkaoni Tabora dhidi ya Rhino Rangers na kuibuka kidedea kwa mabao 3-1.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video