Hawa ni baadhi ya wakazi wa mtaa wa kijitonyama Bwawani wakipanga foleni kutafuta maji ya kununua kwa bei ya shilingi 400 na 500 kwa dumu au ndoo yenye ujazo wa Lita 20.
Sehemu kubwa ya jiji la Dar es Salaam limekuwa sugu kwa ukosefu wa maji inafikia hatua baadhi ya maeneo hununua lita 20 kwa shilingi 700- 800 huku maji ya kisima maarufu kama maji ya chumvi yakiuzwa kati ya
shilingi 300 – 500.
shilingi 300 – 500.


Hata hivyo wakati wengine wakisota na kudai kuwa katika mitaa yao mabomba ya maji hayatoi maji lakini katika mtaa wa Kijitonyama Mpakani B baadhi ya mabomba yamepasuka na kutitirisha maji hovyo mithili ya maji ya mvua huku mamlaka husika zikidaiwa kutoyakarabati mabomba hayo licha ya kudaiwa kupewa taarifa.
PICHA ZOTE NA GERVAS CHARLES MWATEBELA

0 comments:
Post a Comment