
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) akimsikiliza
kwa makini Balozi wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek (kushoto) wakati
walipokuwa wanajadiliana masuala mbalimbali. Balozi huyo ambaye hivi
karibuni anamaliza kipindi chake cha miaka minne ya kuwa balozi nchini
ameishukuru Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano wake. Kulia
ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima.

Balozi
wa Uholanzi nchini, Dk Ad Koekkoek (kushoto) akimshukuru Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi (katikati) pamoja na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima, mara baada ya
kumaliza majadiliano yao yalikuwa yakifanyika ofisini kwa Mhe. Dk
Nchimbi jijini Dar es Salaam. Balozi huyo ambaye hivi karibuni anamaliza
kipindi chake cha miaka minne ya kuwa balozi nchini ameishukuru Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa ushirikiano wake. Picha zote na Felix
Mwagara wa Wizara ya Mambo ya Ndani.
0 comments:
Post a Comment