Kim
Paulsena amesema vijana wake wana morali kubwa sana kukabiliana na timu
bora zaidi barani Afrika, Ivory Coast na leo lazima Taifa stars ipate
ushindi wa nyumbani 

Na Baraka Mpenja
Muda
mfupi kabla ya kushuhudia kipute cha kukata na mundu baina ya timu ya
Taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya Tembo kutoka pwani ya magharibi
mwa Afrika, Ivory Coast, mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la
dunia mwakani nchini Brazil, Kocha wa Taifa Stars, Kim Paulsen
amewahakikishia Watnzania wote kuibuka na ushindi katika mechi hiyo
ngumu ya kundi C.
Akiongea
na mtandao huu, Kim amesema kikosi chake kina morali kubwa kuvaana na
Ivory Coast ambao ni bora zaidi kwa kucheza soka barani Afrika.
“Ivory
Coast ni timu ya kwanza kwa ubora barani Afrika, wachezaji wangu huwa
wanafurahi sana kucheza na timu bora. Imani yangu ni kwamba, vijana
watacheza soka zuri na kuwabamiza wapinzani wetu hao”. Alisema kim.
Kocha
huyo amesema kukosekana kwa wachezaji wake wawili wa kikosi cha kwanza,
Mrisho Ngassa na Agrey Moriss ambao wanatumikia adhabu ya kadi,
kwamaana ya kadi nyekundu kwa Moriss ambapo mlinzi huyo alipata nchini
Morocco huku Ngassa akiwa na kadi mbili za njano, hakutaathiri kikosi
chake kwani kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kufanya vizuri.
“Sio
wakati wa kuzungumzia nani atakosekana, kikosi changu kina wachezaji
zaidi ya Ishirini, leo hii Canavaro ataziba nafasi ya Moriss, lakini kwa
suala la Ngassa bado nina wachezaji wengi wa kuchukua nafasi yake,
ingawa hali hii pia imeniwazisha sana”. Alisema Kim.
Kwa upande wa Nahodha wa Stars, Juma Kaseja ameimbia MATUKIO DUNIANI kuwa wanawaheshimu sana wapinzani wao kwa maana ya ubora wao, lakini hawaogopi kitu kwani wanaweza kufungika katika mchezo huo.
“Ivory
Coast wametutangulia kimchezo, lakini haina maana tunawaogopa, tuko
sawa, tumefanya maandalizi mazuri na leo hii lazima tuibuke na ushindi
ili kuwapa raha mashabiki wetu walioanza kuingia uwanjani”. Alisema
Kaseja.
Kikubwa
Kaseja amewaomba Watanzania kuwaombea dua njema wachezaji wao ili leo
waibuke na ushindi muhimu mbele ya miamba hiyo ya Afrika.
Naye
Nadir Haroub Canavaro amefurahishwa sana na kitendo cha kupata namba
katika kikosi cha kwanza cha Taifa stars katika mechi ya leo.
“Ni
mechi ngumu sana, mimi huwa nafurahi sana kucheza mechi ngumu kwani
inanijengea historia nzuri, hivyo nimefurahi sana kuanza leo na lazima
nicheze kufa na kupona kuisaidia timu yangu”. Alisema Canavaro.
Naye Frank Domayo amesema kuwa mchezo wa leo wamejiandaa kupata ushindi ingawa wanatambua ubora wa wapinzani wao.
“Binafasi
najisikia furaha sana kucheza kikosi cha kwanza katika mchezo wa leo,
nimekuwa nikiimarika sana katika michezo mikubwa, nafikiri leo pia
nitatumia nafasi yangu kuisaidia Stars”. Alisema Domayo.
Kwa upande wa mchezaji nguli wa Ivory Coast, Solomon Kalou ameimbai MATUKIO DUNIANI Kuwa mchezo wa leo ni mgumu sana, lakini Taifa stars bado ni timu ndogo hivyo watafungwa tu.
“Walicheza
vizuri nyumbani na kutupa changamoto, lakini nafikiri bado ni wachanga
sana, tutawafunga ingawa kila timu ina nafasi ya kushinda”. Alisema
Kalou.
Mchezo
wa stars unatarajiwa kuanza majira ya saa tisa alasiri katika dimba la
taifa jijini Dar es salaama na tayari joto la mechi hiyo limeshapanda
vya kutosha huku watu wakiingia uwanjani.
Mchezo wa kwanza Stars walifunga mabao 2-0 jijini Abijan nchini Ivory cOsta mwaka jana.
Kila la kheri stars katika mchezo wa leo.
0 comments:
Post a Comment