Mwenyekiti
 wa Chadema, Mh Freeman Mbowe akiwasili viwanja vya Soweto, Kata ya 
Kaloleni Jijini Arusha jioni ya jana katika Mkutano wa Chadema kufunga 
kampeni zake. (PICHA NA  HABARI  KWA HISANI YA  
http://woindeshizza.blogspot.com/)
 
Mh Mbowe akichangisha pesa mkutanoni hapo sekunde chache kabla ya mlipuko kutokea
Hali ilivyokuwa baada ya mlipuko ulioua na kujeruhi vibaya
Hali za majeruhi na marehemu wakiwa chini kabla ya kukimbizwa hospitalini
  | 
Uwanja wa 
Soweto ambapo Mkutano wa Chadema kufunga kampeni za kuwania Udiwani Kata
 ya Kaloleni Jijini Arusha ulikuwa unafanyika umegeuka kuwa uwanja wa 
vilio baada ya kinachodhaniwa kuwa bomu kulipuka na kuua watu watatu na 
zaidi ya 15 kujeruhiwa vibaya huku baadhi yao wakiwa wamevunjika miguu.  Katika Mkutano huo walikuwapo pia Mwenyekiti wa Chadema naa 
Mbunge wa Arusha Mjini, Mh Godbless Lema sambamba na viongozi wengine wa
 Chadema Mkoa wa Arusha lakini bahati nzuri Mbowe na Lema ambao walokuwa
 vinara katika Mkutano huo hawakudhurika moja kwa moja na mlipuko huo.Mlipuko
 huo ulitokea mbele ya gari ambalo lilikuwa ni jukwaa la matangazo mara 
baada tu ya Mh Mbowe, Lema na viongozi wote waliokuwa jukwaa kuu kushuka
 chini na kujichanganya katikati ya watu wakikusanya michango ya watu, 
hali inayoashiria mrushaji huenda lilenga kuwajeruhi viongozi hao.Miili
 ya marehemu na majeruhi walipelekwa hospitali ya Mt Meru lakini 
hawakupokelewa baada ya kilichoelezwa ni vurumai iliiyoletwa na mamia ya
 wafuasi wa Chadema waliokuwa na hasira baada ya wenzao kuuwawa. 
Baadhi ya majeruhi ni viongozi wa Chadema ngazi ya Kata, 
Wilaya na Mkoa wa Arusha, sambamba na wananchi wa kawaida wakiwemo 
watoto waliofika mkutanoni hapo. | 
 
0 comments:
Post a Comment