
>>UBINGWA, BILA SHAKA, YANGA AU
AZAM!!
>>MWEREKA: 3 KATI YA LYON, TOTO,
POLISI, PRISONS & TIMU ZA JKT!!
>>ZIMEPANDA VPL MSIMU UJAO NI
RHINO, MBEYA CITY & ASHANTI!!
INGAWA, kimahesabu kwenye VPL, Ligi Kuu Vodacom,
kuanzia Timu ya 4 Simba, inayofuata Kagera Sugar, Timu iliyo nafasi ya Pili,
Azam FC, na Vinara, Yanga, ndio wanaoweza kutwaa Ubingwa, lakini ukweli ni kuwa
ni Yanga na Azam ndizo zenye nafasi kubwa kutwaa Taji huku huko mkiani kuanzia Timu
iliyo nafasi ya 7 hadi ya mwisho, nafasi ya 14, ndizo zilizo kwenye balaa kubwa
kuwemo kwenye zile Timu 3 zitakazoshuka Daraja mwishoni mwa Msimu.
Kwa sasa, kuna Timu zimebakisha Mechi 4 kumaliza
Ligi na nyingine Mechi 5 na ni Ruvu Shooting pekee iliyobakisha Mechi 6.
Ugumu wa Mechi na mshikemshike wa kujinusuru
kuporomoka Daraja umeshika moto na katika Mechi za juzi Timu 3 za mkiani,
African Lyon, Polisi Moro na Toto African, zote zilijitutumua na kupata matokeo
mazuri kwao.
Toto Africans waliibana Simba na kutoka sare ya
2-2, Polisi Moro walitoka 0-0 na Yanga na Lyon waliichapa Coastal Union Bao
1-0.
Juu ya Timu hizo 3 za mkiani, zipo Timu 5 zilizo
nafasi za 7 hadi 11 ambazo bado zipo hatarini kuporomoka na zinaweza kuvutwa na
kuwa kwenye eneo la Timu 3 za mkiani na hali hii inaifanya Ligi iwe ngumu na
isitabirike.
Timu 3 za mwisho mkiani ndizo zitashushwa Daraja
mwishoni mwa Msimu na nafasi zake kuchukuliwa na Timu 3 zilizopanda Daraja
kutoka FDL, First Division League, ambazo ni Rhino Rangers ya Tabora, Mbeya
City na Ashanti ya Dar es Salaam.
Rhino Rangers na Mbeya City zitakuwa zikicheza
VPL kwa mara ya kwanza wakati Ashanti wanarudi tena baada ya kuporomoshwa Msimu
uliopita.
VPL inatarajiwa kumalizika Mei 18.
MSIMAMO:
NAMBA
|
TIMU
|
MECHI
|
W
|
D
|
L
|
GD
|
POINTI
|
1
|
YANGA
|
21
|
15
|
4
|
2
|
25
|
49
|
2
|
Azam FC
|
21
|
13
|
4
|
4
|
20
|
43
|
3
|
Kagera Sugar
|
22
|
10
|
7
|
5
|
7
|
37
|
4
|
Simba
|
21
|
9
|
8
|
4
|
11
|
35
|
5
|
Coastal Union
|
22
|
8
|
8
|
6
|
3
|
32
|
6
|
Mtibwa Sugar
|
22
|
8
|
8
|
6
|
2
|
32
|
7
|
Ruvu Shooting
|
20
|
8
|
5
|
7
|
2
|
29
|
8
|
JKT Oljoro
|
22
|
7
|
7
|
8
|
-1
|
28
|
9
|
Mgambo Shooting
|
21
|
7
|
3
|
11
|
-6
|
24
|
10
|
JKT Ruvu
|
21
|
6
|
4
|
11
|
-15
|
22
|
11
|
Prisons FC
|
21
|
4
|
8
|
9
|
-9
|
20
|
12
|
African Lyon
|
22
|
5
|
4
|
13
|
-17
|
19
|
13
|
Police M
|
22
|
3
|
9
|
10
|
-10
|
18
|
14
|
Toto African
|
22
|
3
|
9
|
10
|
-12
|
18
|
**TEBO toka TFF [Tanzania Football
Federation]
RATIBA:
Jumatano Aprili 3
TOTO AFRICANS v TANZANIA PRISONS [CCM KIRUMBA,
MWANZA]
Jumatano Aprili 10
YOUNG AFRICANS v JKT OLJORO [UWANJA WA TAIFA, DAR
ES SALAAM]
TANZANIA PRISONS v MGAMBO JKT [SOKOINE, MBEYA]
POLISI MOROGORO v RUVU SHOOTINGS [JAMHURI,
MOROGORO]
COASTAL UNION v JKT RUVU [MKWAKWANI, TANGA]
MTIBWA SUGAR v FC TOTO AFRICANS [MANUNGU,
MOROGORO]
AZAM FC v AFRICAN LYON FC [AZAM COMPLEX, DAR ES
SALAAM]
Jumamosi Aprili 13
AZAM FC v SIMBA SC [UWANJA WA TAIFA, DAR ES
SALAAM]
MGAMBO JKT v YOUNG AFRICANS [MKWAKWANI, TANGA]
MTIBWA SUGAR FC v JKT OLJORO [MANUNGU, MOROGORO]
TANZANIA PRISONS v RUVU SHOOTINGS [SOKOINE,
MBEYA]
0 comments:
Post a Comment