Na Baraka Mpenja kwa msaada wa Sportsmail.com
Hatimaye
dakika tisini za mchezo wa ligi kuu soka nchini England baina ya
waliokuwa mabingwa wa ligi hiyo Manchester city dhidi ya West Ham United
katika dimba la Etihad zimemalizika kwa kocha Roberto Mancini kuibuka
na ushinidini wa 2-1.
Mabao
ya City yametiwa kimiani na nyota wake Sergio Kun Aguero dakika ya 28
akipokea pasi kutoka kwa mfaransa Samir Nasri na katika dakika ya 83
gwiji la soka kutoka pwani ya magharibi mwa Africa, nchini Ivory Coast,
Yaya Toure akazamisha gozi kimiani.
Wakati
City wakiibuka kidedea leo hii, kocha wake tayari alishasema kuwa
wanatakiwa kufanya usajili mzuri msimu ujao ili kushindana na watani zao
wa jadi mashetani wekundu, Mnchester United.

Bao la kwanza la city likitiwa kimiani na Sergio Aguero huku kipa wa Westenham Jussi Jaaskelainen akiambulia manyoya.

Aguero na Nasri wakishangilia bao la kwanza kwa city jioni ya leo

Yaya Toure akipachika bao la tatu pili na la ushindi

Wachezaji wa Man city wakishangilia bao la Toure

Heshima: Leo mashabiki wa timu za City na Westham walisimam kwa heshima na mpira kusimama katika dakika ya 23 ya mchezo akiwa ni kumbukumbu ya Mcameroon Marc-Vivien Foe aliyefariki uwanjani mwaka 2003

Pablo Zabaleta akipiga shuti na kuokolewa na kipa Jaaskelainen.

Andy Carroll akitia gozi kambani katika mchezo wa leo

Kipa wa city Joe Hart akishangaa mpira ukizama kimiani

Mpira ukiwa nyavuni
0 comments:
Post a Comment