
Na Baraka Mpenja Dar
es Salaam
Mchezaji nguli wa maafande wa JKT
Ruvu, pia aliyewahi kutamba akiwa na wekundu wa Msimbazi Simba, DC Mote Mapembe
ya jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo pamoja na timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
stars, Musa Hassan Mgosi ametamba kuiokoa klabu yake isishuke daraja msimu huu.
Akizungumza katika mahojiano maalumu
na matandao huu, Mgosi ambaye jina lake ni la kibantu likimaanisha mwanaume,
amesema kamwe timu yake haiwezi kushuka daraja kufuatia hali yake kuimarika na
kurudi katika kiwango chake cha kawaida.
“Nilikuwa majeruhi, lakini siku nne
zilizopita nimeanza programu ya mazoezi, najiona kuwa makini, kilichobaki ni
vita ya kukwepa panga la kushuka daraja, na kwa pamoja tutaweza”. Alisema
Mgosi.
Nyota huyo ambaye jina lake haliwezi
kusahaulika kwa wana Msimbazi kutokana na kufunga magoli muhimu, aliongeza kuwa
ligi ya sasa ina ushindani mkubwa sana huku kila timu inaonekana kuwa imara
zaidi inapocheza mechi.
Mgosi aliongeza kuwa yeye ni mchezaji
wa kimataifa na ana uzoefu mkubwa wa kufunga magoli, hivyo lazima aibebe JKT Ruvu
msimu huu ikiwa ni sehemu ya kuilipa fadhila timu hiyo aliyoanza nayo katika
safari yake ya soka.
“Unajua JKT Ruvu ni nyumbani, wengi
walijiuliza kwanini nimeichagua nilipotokea Kongo, kikubwa timu hii ni nyumabi
kwangu, nilianzia soka hapa, nimerejea kuinusuru na lazima ibaki ligi kuu”.
Alisema Mgosi kwa kujiamini.
Akizungumzia ndoto zake za kurudi
timu ya taifa kwa mara nyingine, Mgosi alisema yeye ni mchezaji mwenye imani
mkubwa na nidhamu kubwa ya mazoezi, hivyo ataweza kurudi tena timu ya taifa
inayonolewa na kocha Kim Paulsen.
Mgosi alisisitiza kuwa timu ya taifa
ya sasa ina wachezaji wazuri, wanapata huduma zote kutoka kwa wadhamini, hivyo
anatamani kurudi ili alitumikie taifa kwa moyo wote.

Maafande wa JKT Ruvu wapo hatarini
kuaga michuano ya ligi kuu, kwani mpaka sasa wamejikusanyia pointi 22 wakiwa
nafasi ya 10 kati ya timu 14 za ligi hiyo.
Jumatano ya Aprili 10 watakuwa
ugenini katika dimba la CCM Mkwakwani Mkoani Tanga “waja leo waondoka leo”
kumenyana na wagosi wa kaya Coastal union.
0 comments:
Post a Comment