Saturday, April 6, 2013


Yanga au Simba?Aggrey Morris Ambroce katika picha mbili tofauti;

BEKI wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Aggrey Morris Ambroce yuko mbioni kujiunga na klabu ya Yanga ya Dar es Salaam, imebainika.
Morris ambaye kwa sasa amesimamishwa na klabu yake kwa tuhuma za kuijuhumu katika mechi dhidi ya Simba SC mzunguko wa kwanza Ligi Kuu, inaelezwa amekwishafanya mazungumzo na uongozi wa Yanga na kufikia makubaliano.
Habari za ndani ambazo zimepatikana, zinasema kwamba Morris mwenyewe ameonyesha nia ya dhati ya kwenda kuvaa jezi za kijani na njano msimu ujao.
Hata hivyo, wakati Morris akiwa amefikia makubaliano na Yanga, kuna habari kwamba klabu yake inaweza ikamtoa kwa mkopo kwenda Simba SC akamalizie mkataba wake huko.
Hiyo inatokana na Azam FC kumtaka kiungo Mwinyi Kazimoto wa Simba SC ambaye naye kwa sasa amevurugana na klabu yake hiyo.
Simba inaonekana ipo tayari kumtoa Kazimoto, lakini ipewe mabeki wawili, Erasto Nyoni na Morris ambao wote wamesimamishwa hivi sasa kwa tuhuma za hujuma.
Kubadilishana itawezekana? Erasto Nyoni kulia na Mwinyi Kazimoto kushoto

Na Azam inaonekana pia kuwa tayari kuwatoa wawili hao, ili iimarishe safu yake ya kiungo kwa kumsajili Mwinyi.
Lakini habari zaidi zinasema, katika suala la Mwinyi baadhi ya Wakurugenzi wa Azam hawamtaki mchezaji huyo kwa madai amekwishaingia kwenye kashfa ya utovu wa nidhamu, hivyo wanahofia atawasumbua.
Lakini pia inaelezwa rekodi za wachezaji waliosajiliwa kutoka Simba na Yanga baadaye kuisumbua klabu hiyo, nayo inatia uzito suala la usajili wa Mwinyi.
Mrisho Khalfan Ngassa alisajiliwa Azam kutoka Yanga, lakini baadaye akaibusu jezi ya Yanga akiwa klabu hiyo ya Said Salim Bakhresa na familia yake.
Ramadhani Chombo ‘Redondo’ alisajiliwa Azam kutoka Simba SC na baadaye akaamua kurudi tena klabu yake bila kuomba ridhaa wala kuzingatia mkataba wake.
Kwa hayo na mengine mengi ya ndani, baadhi ya Wakurugenzi wa Azam wanaona si busara tena kuendelea kusajili wachezaji kutoka Simba na Yanga na badala yake ni bora kutafuta wachezaji kutoka timu nyingine kabisa.
Ikumbukwe Nyoni na Morris ni kati ya wachezaji wanne wa Azam waliosimamishwa mwishoni mwa mwaka jana kwa tuhuma za kuihujumu timu hiyo ikafungwa 3-1 na Simba SC, wengine wakiwa ni kipa Deo Munishi ‘Dida’ na beki Said Mourad.
Tayari suala hilo lipo kwenye meza ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wachezaji wote wamekwishahojiwa.
Aidha, wachezaji wote hao kwa sasa hawana nafasi tena Azam baada ya wapya waliosajiliwa, David Mwantika na Mkenya Joackins Atudo kuziba nafasi zao vyema.    

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video