Katibu mkuu wa klabu hiyo, Sadick Jumbe, amesema wachezaji wote wanaendelea kujiweka "fiti' huku kila mmoja akionesha nia ya kuchaguliwa na kocha mkuu Jumanne Chale katika kikosi cha kwanza cha amaafande hao.
MASHABIKI WA TANZANIA PRISONS YA JIJINI MBEYA WAKIWASHANGILIA WANANDINGA WAKE |
Jumbe amesema mchezaji wao nyota na mkongwe Emmanuel Gabriel Mwakyusa anaendelea vzuri kunoa makali yake na anaonesha kiwango cha hali ya juu sana, kitu kinachowatio moyo kuwa lazima watafanya vizuri na kupata angalau nafasi mojawapo katika timu nne za juu.
 Pia ameongeza kuwa mzunguko wa pili wataanza na mabingwa wa soka kwa ukanda wa afrika mashariki na kati kwa kombe la vilabu, Dar Yanga africans ya Dar es salaam mchezo utakaochezwa uwanaja wa taifa Dar es salaam.
Wapinzani hao wa kwanza wa Prisons wapo kujifua nchini Uturuki na wanajiandaa vilivyo chini ya kocha wake Ernest Brandits akisaidiana na msaidizi wake Fred Felix Minziroo.
0 comments:
Post a Comment