Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake Tanzania (TWFA)
kimetoa tuzo kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar
Tenga na Meneja wa timu ya Taifa (Twiga Stars), Furaha Francis kutokana na
mchango wao katika kuendeleza mchezo huo.
![]() |
RAIS WA TFF, LEODIGAR TENGA |
Tuzo hizo zilitolewa katika Mkutano wa Uchaguzi wa
TWFA uliofanyika Desemba 19 mwaka huu mjini Morogoro kutokana na mchango wao
katika kuendeleza mpira wa miguu kwa wanawake nchini.
“Ni dhahiri kazi ya kuendeleza soka ya wanawake ni
wajibu wa Shirikisho (TFF), lakini Rais wa TFF alitoa kipaumbele zaidi na
alijitoa kuhakikisha misingi imara ya kuendeleza soka ya wanawake inawekwa,”
alisema Mwenyekiti wa TWFA, Lina Kessy.
Pia Mkutano huo ulitambua na kumpa tuzo Furaha Francis
ambaye amekuwa Meneja wa Twiga Stars kwa miaka minane mfululizo. Licha ya kuwa
Meneja wa Twiga Stars, ametumia muda wake na kujitoa katika kuendeleza mpira wa
miguu kwa wanawake.
TWFA itaendelea kutumia michango yao katika mpira wa
miguu kwa wanawake nchini.
0 comments:
Post a Comment