Monday, December 31, 2012

 

DR. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA


LEO Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kote kusherehekea mwaka mpya wa 2013.
Hizi ni sherehe kubwa, ambazo hakika watu wengi huzisubiri kwa hamu kubwa, ikiwa ni pamoja na kuzitumia kama tathmini ya nini wamefanya kwa kipindi chote cha miezi 12, hivyo kujiwekea malengo katika mwaka mpya.
Kwetu Tanzania, mwaka 2012 bila shaka umekuwa na changamoto nyingi za hapa na pale, ukiachilia mbali mafanikio yaliyopatikana kwa kila mtu mmoja mmoja na kwa pamoja kama taifa.
Lakini tunaweza kujikumbusha machache kama vile kushamiri kwa matukio ya ujambazi, mmomonyoko wa maadili, matumizi makubwa ya dawa za kulevya, ajali za kila aina, rushwa, mauaji, ubadhilifu na mengine mengi.
mmomonyoko wa maadili
Madawa ya Kulevya
watu wakiangalia washukiwa wa ujambazi

Haya mambo kimsingi hatuwezi kuyamaliza kwa wakati mmoja, lakini kwa kujiwekea mikakati kama taifa na kuazimia, tunaweza kuyapunguza na mengine kuyakomesha kabisa.
Suala hapa ni uwajibikaji wa pamoja na uzalendo kwa taifa. Ndiyo maana katika kusherehekea sikukuu hii ya mwaka mpya wa 2013, ni heri tukautumia mwaka huu ukawa wa vitendo zaidi kuliko maneno.
Kwa bahati mbaya sana mambo yetu mengi yanafanywa kisiasa, sheria hazitekelezeki kwa wote, hatua hazichukuliwi kwa wanaokiuka utaratibu halafu mwishowe tunakiri kushindwa hata yale yanayowezekana wazi.

Hatutaki kukosolewa, tunapenada kulalamika tu pasipo kila mmoja kutimiza wajibu wake kwanza. Kumbe mwaka huu tukiuweka kwenye vitendo zaidi tunaweza kufanikiwa.

Mwaka huu uwe wa kukumbuka kauli ya Rais mstaafu wa Marekani, John F. Keneddy, kwamba kila mtu ajiulize nini amefanya kwa ajili ya nchi yake, badala ya kuhoji nchi itamfanyia nini.
Kwa utaratibu huu itatusaidia sana hata kufanya mambo mengi makubwa kwa juhudi na uwezo wetu wenyewe badala ya kutegemea wafadhili wa kigeni kutoa fedha.

Kama tunaweza kuchangia harusi ya siku moja kiasi cha sh milioni 15 za watu kula na kunywa, tutashindwaje kujitutumua kuchangishana watoto wetu wakaenda shule kwa faida yao maishani?

Tubadilike sasa na tuutumie mwaka 2013 kwa kufanya vitendo zaidi, tupunguze mijadala ya siasa, tuache kulalamika hata kwa makosa tunayoyasababisha wenyewe, hatimaye tutafika kwenye malengo.

Heri ya mwaka mpya 2013. Tuhakikishe tunaondokana na uzembe wa kukata tamaa na kushindwa kabla ya kuanza, kila mmoja atimize wajibu wake, hakika tutafanikiwa.

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video