
Ametoa kauli hiyo leo mchana
(Jumanne, Desemba 25, 2012) wakati wa ibada ya Krismasi iliyofanyika
katika kigango cha Kibaoni kata ya Kibaoni wilayani Mlele, mkoani
Katavi.
“Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa
kutuwezesha kufika sikukuu hii, mpaka leo ni mapenzi yake hakuna
binadamu ambaye ana amri na maisha yake. Tutakumbuka hata mwaka jana
tulikuwa na Askofu wetu wa Jimbo la Mpanda lakini leo hii hatunaye,
hivyo sote tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutupa uhai,” alisema.
Alisema katika kuadhimisha
sikukuu hii watu hawana budi kuwa na kiasi, wasinywe sana hadi
kusababisha magomvi. Aliwasihi wazazi wawe karibu na familia zao, na
wawajibike kwao.
”Tumuombe Mungu atupe neema,
yale tuliyokosea mwaka 2012 tuyaache, tujiandae kuingia mwaka 2013 na
yale mazuri tuliyoyaona mwaka 2012,” alisema.
Naye Padre John Giji wa Shirika
la Wamisionari wa Mt. Thomas ambaye aliongoza ibada hiyo, aliwataka
waumini wa kigango hicho kuwajali wenye shida na siyo kujiingiza katika
matendo mabaya wakati wa sikukuu.
“Kuishi kwetu kuanzia leo lazima
kuwe na mabadiliko, ni lazima tuwajali wenzetu katika shida zao kwani
kwa kufanya hivyo, tutakuwa na mabadiliko ya kiroho na hivyo kuweza
kukua kiimani,” alisema Padre John ambaye pia ni Paroko wa Usevya.
“Wako watu wanasherehekea
Krismasi kwa matendo mabaya kama vile uzinzi na ujambazi. Huo siyo
ukristu tunaotegemewa kuwa nao katika familia takatifu ya Mungu.
Tukifanya kazi kwa bidii, hatuwezi kuwa na tamaa ya vitu vya wengine,”
alionya.
“Leo ni sikukuu, tufurahi kwa amani bila jazba za kidunia. Tusherehekee kwa upendo na amani, ” alisisitiza.
0 comments:
Post a Comment