
Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba (MB) akiwa na wachezaji wa Yanga ambao wapo mjini Shinyanga kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao dhidi ya Stand United utakaofanyika Uwanja wa Kambarage. Licha ya kuwa kujihusisha na masuala ya siasa Mwigulu ni moja ya mawaziri wanaopenda sana michezo nchini na amekuwa mpenzi mkubwa wa klabu ya Yanga.
Amekuwa akiichezea Yanga kwenye michezo inaowahusisha wabunge wa Simba na wale wa Yanga. Kutokana na kupendelea nafasi ya ushambuliaji amekuwa akifunga magoli mengi.
0 comments:
Post a Comment