Tuesday, September 20, 2016

Wakala wa Mario Balotelli Mino Raiola amesema kuwa anaamini ipo siku Balotelli atarejea kucheza soka katika Premier League.

Mino Raiola ambaye ni wakala wa wachezaji wengi mastaa katika ligi tofauti akiwepo Paul Pogba na Zlatan Ibrahimovic ametanabaisha hayo kutokana na ubora wa kiwango cha Balotelli akiamini bado ana uwezo mkubwa wa kucheza katika timu kubwa. 

Kwa nyakati tofauti Balotelli ameshacheza kwenye Premier League katika vilabu vya Manchester City na Liverpool ambapo amepitia hali tofauti-tofauti.
 
Raiola amenukuliwa akisema: "Ufaransa inamhitaji kama walivyokuwa wakimhitaji Zlatan (Ibrahimovic). Yupo vizuri lakini ipo siku atarejea Premier League."

Balotelli alitua Nice baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na meneja wa Liverpool, Klopp ambaye aliwekaza wazi kuwa hamuhitaji katika kikosi chake.

"Mario na Jurgen Klopp hawakupata nafasi kwa kuwa Klopp hakutaka kumpa nafasi,"  alisema Raiola na kuongeza. "Klopp alikuwa akimuona Balotelli kama mpuuzi tu.”

0 comments:

 
https://www.sexmutant.com/ https://www.sexindrag.com/ porn movies sex videos hd porno video