
Manchester United chini ya Jose Mourinho imepokea kipigo kwa mara ya tatu mfululizo baada ya kushuhudia ikifungwa mabao 3-1 dhidi ya Watford, mchezo wa Ligi Kuu ya England uliochezwa kunako Uwanja wa Vicarage Road maskani kwa Watford.
Wafford walikuwa wa kwanza kupata bao kwenye dakika ya 34 lililofungwa na kiungo mshambuliaji wao Etienne Capoue.
Dakika ya 62 mshambuliaji kinda wa Man United Marcus Rashford alisawazisha bao baada ya mabeki wa Watford kushindwa kuokoa kichwa alichopiga na mpira kumrudia tena na kuukwamisha mpira wavuni.
Waford walipata bao la pili kupitia kwa mshambulaiji wao aliyetokea benchi Juan Camilo Zuniga mnamo dakika ya 84 na kuwachanganya kabisa United.
Wakiwa bado wanajiuliza namna gani ya kusawazisha na pengine kuongeza bao, United walijikuta wakiruhusu bao la tatu lililofungwa na Troy Deeney kwa mkwaju wa penati dakika ya 90 baada ya Fellaini kumchezea madhambi Zuniga.
Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa Mourinho kupoteza michezo mitatu mfululizo ya ligi kwenye msimu tangu ilivyotokea Februari 2002, wakati huo akiwa meneja wa Porto.
0 comments:
Post a Comment